Serikali inauza viwanja mpaka laki 2 maeneo ya Kibaha na - TopicsExpress



          

Serikali inauza viwanja mpaka laki 2 maeneo ya Kibaha na kwingineko Tanzania, lakini ajabu vijana tumekunja nne katikati ya Majiji ya nchi hii tunachezea Iphone 10 ya milioni 4 huku tukisubiri toleo la Galaxy S 20! Like parent,like Child, Baadhi ya wazee wetu nao ndio wale wale, kutwa kuisifia Sinza kwamba zamani ilikuwa pori la Nyani, na wakakataa kununua Viwanja Mbezi beach kwamba ni Kambi ya Sokwe, Na leo watafika mbali kwa stori za kwamba walikuwa wakicheza bado na Bakhressa pale Mtaa wa Swahili huku wakimshuhudia Mr Mengi kabeba Vitabu anasoma CPA pale NBAA. Ndipo wazee hawa wakalala kwenye rumba pale ukumbi wa DDC Kariakoo kabla ya kuamka 21st Century kukera Wajukuu na hadithi hizi za Magazijuto (-gazi), any way kununua Ipad kabla ya Shuka ni Uamuzi tu.
Posted on: Fri, 05 Jul 2013 09:33:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015