Simulizi za Kalibonge Barua ya Halima (13) Ilipoishia - TopicsExpress



          

Simulizi za Kalibonge Barua ya Halima (13) Ilipoishia jana... Nikatembea hatua kadhaa kutoka kwenye nyumba ya mama Egla, nikakutana na taxi. “Niwahishe Ubungo kaka yangu.” Nikamuamuru dereva, naye bila hiyana akaniwahisha Ubungo ambako nilitaka kupanda basi, tayari kurudi nyumbani Dodoma. ********** Endelea... Namaliza kusoma karatasi ya kwanza, yaani kurasa mbili za kwanza huku nikiwa na kurasa mbili za mwisho. Nageuka pale nilipo najikuta niko katikati ya watu wale niliokuja nao hapa makaburi, na namuona Jemedari uzalendo umemshinda, analia kwa sauti na namuona kaka yake mkubwa, Sufiani anamshika kichwa na kumsuka suka kama mama afanyavyo kwa mtoto wake aliyelilia peremende wakati hakuwa na hela ya kumnunulia. Mwenyewe nilijua nasoma kimya kimya barua hii, kumbe haikuwa hivyo, nilisoma kwa sauti hata hawa watu wakasikia na kunizunguka huku wakiwa na shauku kujua kilichoandikwa baruani. Nawaangalia vizuri watu hawa halafu namuona mzee Daud akiwa kimya sana na mwenye kuzama kwenye tafaakuri nzito. Anageuka kunitazama, anakuta nami namtazama, tunatazamana kwa nukta kadhaa hata naona haya na kuyabetua macho yangu na kuangalia chini. Naangalia chini kwa nukta chache halafu nainua kichwa kumuangalia tena mzee Daud, bado ananiangalia, macho yake yanawaka kama nyoka na yanatisha. Hasira! Ameghadhibika sana, lakini sifahamu kwa nini ameghadhibika, au pengine kutokana na kiherehere changu cha kusoma barua kwa sauti badala ya kusoma kimoyomoyo. Najaribu kuyabandua macho yangu ili nisimuangalie mzee Daud, lakini nashindwa. Macho yanakuwa kama yametiwa gundi na ngozi ya juu ya jicho imeshikana kwani hata kupepesa macho nashindwa. Kha! Mambo haya yamekuwaje? Najiuliza na sipati jibu. Bado tunaangaliana na mzee Daud, halafu namuona akifanyia ishara ya kichwa kama mtu anayeitikia ama kukubali jambo aliloambiwa. Simwelewi na anagundua mshangao wangu. Sasa nagundua baada ya kuirudia mara kadhaa ile ishara yake, kumbe ananiambia niendelee kuisoma ile barua, yaani karatasi iliyobakia nao wako tayari kunisikiliza. Nakubaliana naye kwa kichwa pia, halafu kabla ya kuinamisha kichwa kwenye barua, napenga kamasi jembamba. Sasa nainama tena na kuiweka tayari karatasi hii, naanza kusoma ukurasa wa tatu. ******************** Nikafika Ugungo majira ya saa nne asubuhi na sikuchelewa, nikaingia ndani moja kwa moja hadi kwenye basi ambalo ndiyo lilikuwa linatoka. Sikujali kama nitapata siti ama la! Nilichoangalia zaidi ni kuondoka mjini Dar na kuelekea nyumbani na nilijua zilikuwa mbio za sakafuni tu ambazo zina mwisho wake. Jambo nililolifanya halikustahili kufanywa siyo nami tu ila na mtu yeyote hakupaswa kufanya, lakini nilikuwa na sababu ya kufanya hivyo; nimebakwa, nimejazwa mimba na zaidi nimeambukizwa virusi vya UKIMWI, ni wazi maisha yangu yameshaharibika. Siku zangu za kufa zilihisabika na matumaini ya kuishi yalishakwisha na sikutaka kufia katika mikono ya mama Egla ila nyumbani kwetu; kwa wazazi wangu baba na mama na kaka zangu niliowapenda sana. Japo wakati huu sikuwa na thamani tena kwao, lakini niliwahitaji sana. Hao watanitafuta na sehemu ya kwanza kunitafutia itakuwa nyumbani kwetu, hivyo kukimbilia huku haikuwa ni kuukwepa mkono wa dola, hapana. Nilifahamu dola ina mkono mrefu na jicho kali sana linaloweza kuona kila sehemu. Nilitaka nifike kwanza nyumbani, niwaeleze wazazi wangu na kaka zangu na wakija kunishika basin a iwe hivyo wakati ndugu zangu wanaufahamu ukweli. Nikaingia kwenye gari na bahati ikawa upande wangu, palikuwa na kiti kimoja ambacho kilikuwa tupu, nikalipa nauli kisha nikakaa raha mustarehe na safari ikaanza huku nikiwa na matumaini makubwa ya kunyongwa ama kufungwa maisha pindi nikitiwa mikononi mwa serikali. Garini mulikuwa kimya sana, zaidi ya muungurumo wa injini na msuguano wa tairi la lami, hapakuwa na mtu aliyesemezana na mwingine. Ukimya huu kwangu ulikuwa kama ishara ya kufika mahali nisipowahi kufika na ambapo watu hufika lakini hawarudi, yaani mtu akifika katika sehemu hiyo, basi harudi tena. Nikayakumbuka maisha ya siku za kwanza pale kijijini kwetu. Tuliishi maisha ya shida sana lakini yaliyojaa upendo na amani. Nikawaona wazazi walivyotulea katika misingi ya kuheshimiana, kupendana, kuthaminiana na kujaliana. Makuzi yetu yalivyotawaliwa na shida nyingi na namna tulivyokosa kusoma ilcha ya kufaulu darasa la saba kutokana na wazazi wetu kushindwa kumudu gharama za shule. Nikamuona kaka Sufiani alivyojitahidi kuwa karibu yetu huku akifanya kila aliloweza na akipata shilingi kumi mbili, basi akatugawia mimi na Jemedari. Namna alivyorarua suruari yake na shati akampa Jemedari. Taratibu nikajikuta natokwa machozi na kulia moyoni kwa uchungu sana. Nikalia hata yule niliyekaa naye akaniuliza. “Binti vipi, mbona unamwaga machozi?” “Hapana mzee wangu.” Nikamudu kumjibu ingawa alionesha kutoridhika na jibu langu, lakini ikawa dawa kwani hakuniuliza tena. Tukaingia Morogoro majira ya saa saba unusu adhuhuri. Nikateremka lakini sikwenda kula, badala yake nikanunua maji chupa kubwa, nikanawa usoni kisha nikarudi tena garini kusubiri safari. *********** Halima yuko ndani ya gari anarudi nyumbani kwao, Dodoma. Je, atafika aendako?. Unafikiria nini? Andika ubashiri wako hapo chini na usikose kuifuatilia simulizi hii ya kusisimua hapo kesho!. Tunawatakia siku njema___
Posted on: Wed, 07 Aug 2013 02:25:42 +0000

Trending Topics



ght:30px;">
A garota bonita que eu conheço não é nenhuma miss, nem engata
Pepe Auth Go in an elevator and the next person who enters, stare
#Nmeka_the_troublesome_spirit
The other Day Jason Paul Gilbert posted a Video of bagua, and for

Recently Viewed Topics




© 2015