Simulizi za Kalibonge Niliacha shule ili niwe mganga - TopicsExpress



          

Simulizi za Kalibonge Niliacha shule ili niwe mganga (46) Ilipoishia jana... Nikaipokea na kuelekea kwa mhasibu na baada ya kupewa fedha zangu nilitoka na kukutana na yule dereva ambaye nilimpa fedha yake shilingi laki tatu unusu kulingana na mapatano yetu halafu nikamuomba anisindike nyumbani kwani sikuweza kwenda peke yangu huku nikimuomba pia ampigie simu kaka kumtaarifu jambo hili. Endelea.... Simu ilikuwa inaita tu juu ya meza, niliisikia lakini vile nilivyokuwa nimelala pale kitandani, ndivyo vivyo hivyo, sikuweza kufanya chochote zaidi ya kupepesa macho tu. Siyo kama nilikuwa naidharau, la! Sikuweza hata kujitikisa pale nilipolala na zaidi ya kupepepsa macho, basi sikuweza kuinua wala kuweza kutikisa japo kidole kimoja. Nilijaribu kufanya hivyo, lakini nilishindwa; ingawa akili iliweza kufanya kazi, lakini mwili wote ulikuwa mzito sijapata kuona, sikuweza kujigeuza wala kugeuza kichwa kulia ama kushoto. Simu iliendelea kuita, ikakata; ikaita tena pia ikakata. Mpigaji naye hakuchoka, alipokaa dakika kadhaa, akapiga tena lakini ilikuwa kama hapo awali. Moyoni niliumia sana, lakini sikuwa na namna ya kufanya. Pale kitandani nilikuwa kama nimefungwa kamba mwili mzima ama nimetiwa gundi. Nilivyolala ilikuwa hivyo hivyo. Hii ilikuwa ni baada ya kuingia ndani mara tu yule dereva aliponiteremsha pale barabarani tukitokea kwa Bakhresa mishale ya saa tano hivi asubuhi. Niliingia moja kwa moja ndani na kuziweka zile fedha kabatini halafu simu nikaitupia juu ya meza nami nikajitupia kitandani huku nikilalia mgongo na mikono nikiipitisha chini ya shingo na kuilalia badala ya mto huku nikiangalia juu-darini. Basi nilivyolala hivi ndiyo nikawa hivyo hivyo na kila nikijaribu kujihudumia lakini sikuweza. Nikajaribu kuitoa mikono kule chini ya shingo lakini sikuweza, nikajaribu kujitikisa, pia sikuweza; kujigeuza, nako mtihani kadhalika. Sikujihisi kama nina mwili kwani ulikuwa haufanyi kazi, yaani zaidi ya macho na akili kufanya kazi, hakuna kiungo chochote kilichofanya kazi. Nikabaki hivyo. Niliweza kukisia kuwa ilikuwa ni majira ya saa tisa ama kumi hivi alasiri, ndipo nikasikia mtu akibisha hodi mlango. Nikajaribu kuitikia lakini kumbe kinywa nacho kilikuwa kama viungo vingine, kiligoma kufanya kazi kabisa. Yule mgongaji akagonga tena na alipokosa majibu, akajaribu kuusukuma mlango, nao ukaitika. Nakumbuka kuwa sikuufunga, akaingia hadi sebuleni huku akiita, “Bilal! Bilal! Bilal!” Lakini hakujibiwa. Sasa niliisikia sauti ikiita huku ikisogea karibu na mlango wa chumba changu. Bado hakupata majibu naye hakuchoka kuita huku akisogea taratibu na mwishowe akaingia chumbani. “Aakh! Bilal imekuwaje?” Alikuwa ni kaka. Alishtuka aliponiona katika hali ile. Alikuja moja kwa moja pale kitandani na kukaa kwenye ukingo wa kitanda. “Bilal, vipi? Kimetokea nini?” Kama vile mwehu, alikuwa anauliza maswali mfululizo-maswali ambayo nilitamni kuyajibu lakini nilishindwa. Nilimsikia vizuri sana lakini sikuweza kumjibu. Alipoona niko vile vile akachanganyikiwa sana asijue la kufanya. Mara kama aliyetoka usngizini, aliingiza mkono mfukoni na kutoa simu kisha akabonyeza namba kadhaa kabla ya kuibandika sikioni. “Eeenhe! King, uko wapi?...nakuoma uje hapa Kurasini kwa Bilal, haraka sana kuna tatizo.” Alipomaliza kuongea maneno hayo, alikata simu na kuirudisha tena mfukoni halafu akarudi kukaa pale kwenye ncha ya kitanda. Akaniangalia sana hata nikamuona akidosha machozi bila kujijua na kamasi jembamba likamtiririka hata akapenga na kujifuta kwa kiganja cha mkono wa kushoto. Dakika ishirini baadaye simu yake ikaita, akaitoa mfukoni na kuipokea halafu akaibandika sikioni. “Ndiyo King…ingia ndani, njoo huku chumbani kabisa.” Baada ya kuongea hivyo, aliirudisha simu mfukoni, halafu nikasikia sauti ya mtu ikibisha hodi huku akiingia moja kwa moja chumbani bila kusubiri ruhusa. “Hodi!” “Karibu King!” “Asante. He! imekuwaje?” “Mwenyewe nimekuja hapa nimemkuta viyo hivyo. Sijui amekutwa na kitu gani.” King alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na tulikutana pale taifa katika mazoezi ya mpira wa miguu na tuliishi mtaa mmoja, lakini shughuli zake zilikuwa bandarini. Alipoambiwa hivyo akanisogelea pale kitandani. Akaniangalia kwa makini sana, halafu akarudi kusimama karibu na kaka. “Huyu nadhani amekumbwa na pepo.” “Amekumbwa na pepo?” Kaka akauliza. “Ndiyo! Amekumbwa na pepo. Hii siyo homa ya kawaida ndugu yangu. Yaani mtu augue muda mfupi hivi halafu asiweze hata kuinua kidole!” “Kwa hiyo tunafanyaje ndugu yangu?” Akauliza kaka. “Ngoja, yupo mtaalamu mmoja hivi hapo mtaa wa nyuma, hebu nikamuangalie.” Akasema King baada ya kutafakari kwa nukta kadhaa, kisha akatoka nje mbio. Jua lilikuwa lieanza kutua katika makao yake ya usiku. King akaingia na mtu mmoja ambaye baadaye niligundua kuwa alikuwa imamu wa msikiti wa mtaa wa pili ambako nilikwenda kuswali Ijumaa moja moja. Yule imamu alikuja moja kwa moja hadi pale kitandani na aliponiona tu akaropoka. “Muda waliompa umefikia mwisho hivyo wanamtaka.” Kaka na King wakatazamana usoni kabla ya kumgeukia yule imamu. “Kwani bado tu walikuwa na nia naye?” Akauliza kaka. “Huyu walimhitaji tangu zamani na walimpa muda wa kukua na sasa amefikia hatua waliyoitaka, hivyo hapa hakuna ujanja zaidi ya kukubali tu.” Akasema imamu. King alikuwa njia panda hata akauliza, “Kulikoni jamani mbona sijawaelewa hapo?” Kaka akaanza kumsimulia kisa kizima hata King akastaajabu sana. Yule imamu akasema, “Hapa tutafanya kisomo kimoja tu ambacho kitakuwa ni kwa ajili ya kuwaomba wamfungue mwili.” Alipokwishasema hivyo akaondoka huku akiahidi kurudi baada ya muda mfupi ujao. ***************** Baada ya mambo kumuendea kinyume na matarajio yake, Bilal yuko hoi kitandani. Je, nini hasa? Tukutane kesho!. Tunawatakia siku njema___
Posted on: Tue, 16 Jul 2013 05:37:03 +0000

Trending Topics



ody" style="min-height:30px;">
Successful day: FaceTime with Stephanie Watts, Avila Barn for
Training and Development in NB Twin Prop Productions is a film and
I saw Susie sitting in a shoe shine shop. Where she sits she
?? ARE YOUR TWITTER TWEETS BRINGING YOUR PROSPECTS INTO YOUR
Shamrock Shuffle will host USATF Natl Club Team 8k champs, by
Our stint in our Home is coming to an end. Tonight is our last
Federal government yesterday announce a new automobile scheme that

Recently Viewed Topics




© 2015