Siri ya Dr.Slaa na Dr.Ayub Rioba kuwa na msimamo sawa kuhusu - TopicsExpress



          

Siri ya Dr.Slaa na Dr.Ayub Rioba kuwa na msimamo sawa kuhusu Amani Awali ya yote, natumia jukwaa hili kuwapongeza wana UDASA kwa kongamano safi kwa maslahi ya taifa letu, bila shaka mjadala unaendelea na sasa hapa fb tuangazie; amani huletwa au huvurugwa na nini? Mengi yamezungumzwa, lakini mimi hoja zangu nitazielekeza kwa wasomi wawili waliotoa mitazamo sawa kuhusu mantiki ya amani. Dr.Willibrod Slaa na Dr.Ayub Rioba, hoja yao ni moja tu katika hili yaani "amani haihubiriwi,haiombewi wala haitekelezeki kama sera bali haki ni sera ya amani". Wapo wanaowachukulia wasomi hawa kama wasaliti wa amani, lakini mimi nawaona ni marafiki wa amani. Tufikiri, ni amani huleta haki au haki huleta amani? Kama haki huleta amani, bila haki hakuna amani, hivyo haki ni amani. Ndivyo waonavyo wawili hawa na wengine wenye mtazamo kama wao. Kwa mantiki hii, Kama msimamo wa Mhe.Mwigulu na Mhe.Nchimbi kuhusu kuombea amani kuna hoja, naomba tujadili maana hata Syllogism argument haipo!
Posted on: Mon, 29 Jul 2013 08:56:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015