Supasta alipopata mkwanja akaamua kuhamia mitaa ya watu wenye pesa - TopicsExpress



          

Supasta alipopata mkwanja akaamua kuhamia mitaa ya watu wenye pesa akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae alipokuwa anacheza na manati akavunja kioo cha nyumba ya jirani. Supastar na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafungua mbaba mmoja;MBABA: karibuni SUPASTA: Samahani sie tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza MBABA: Karibuni kwenye kiti niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi. Mimi ni ZIMWI nilikuwa nimefungiwa kwa zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa kilikuwa kwenye kile chumba ambacho dirisha limevunjwa, chupa nayo imevunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa SUPASTAA:Mi naomba niwe bilionea mpaka nife MBABA: Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho utaamka tajiri MKE WA SUPASTA: Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong MBABA:Umepata kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina ombi dogo. SUPASTAA: Sema tu MBABA: Mi naomba nilale na mkeo leo tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu. Asubuhi ikifika hamtaniona tena, itakuwa siri yetu Supasta na mkewe wakajadili, wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana hilo jambo ni dogo wakakubali sharti. Mke akalala kwa Mbaba mpaka asubuhi. Wakati mke akijitayarisha kurudi kwake Mbaba akakohoa kidogo; MBABA: We una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?? MKE: Mume wangu 32 na mimi 30 MBABA: Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za MAZIMWI?
Posted on: Thu, 22 Aug 2013 08:54:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015