Sénégal ni nchi ya Afrika ya Magharibi… Imepakana na - TopicsExpress



          

Sénégal ni nchi ya Afrika ya Magharibi… Imepakana na Mauritania upande wa kaskazini, Mali upande wa mashariki, Guinea-Conakry na Guinea-Bisau upande wa kusini na Bahari Atlantiki upande wa magharibi… Nchi ya Gambia iko ndani ya eneo la Senegal... Visiwa vya Cape Verde viko 560 km mbele ya pwani la Senegal. Senegal ilikuwa koloni ya Ufaransa hadi 1960... Ilipata uhuru August 20,1960… Rais wa Senegal wa sasa ni Macky Sall, mji mkuu wa nchi hiyo ni Dakar… Lugha za taifa ni Diola, Malinké, Pular, Sérère, Soninké na Wolof… Lugha rasmi ni Kifaransa… Hiyo jana basi, wananchi wa Senegal walisherehekea miaka 53 ya uhuru wa taifa lao. Napenda kutumia fursa hii kuwatakia wajukuu zangu wote, raia wa Senegal, sikukuu njema ya uhuru wao, hususan huyu mjukuu wangu wa karibu sana, Assane Diop akiwa pande za Dakar… Mungu ibariki Senegal, Mungu ibariki Afrika!!!...
Posted on: Wed, 21 Aug 2013 10:19:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015