TAARIFA MPYA KUTOKA VODACOM KUHUSU TATIZO LA MTANDAO HAPO JANA - - TopicsExpress



          

TAARIFA MPYA KUTOKA VODACOM KUHUSU TATIZO LA MTANDAO HAPO JANA - Baadhi ya maeneo mtandao umerudi katika hali ya kawaida. - Wateja kurejeshewa huduma zote za vifurushi walizokuwa wamezinunua hapo jana. Moto uliozuka jana katika mitambo ya kuendesha mtandao (switch) wa Vodacom na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya mtandao wa Vodacom ulizimwa jana jioni. Akizungumza jioni hii Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom, Georgia Mutagahywa alisema moto huo ulipelekea kusimama kwa huduma zote za kampuni hiyo. "Tunawaomba radhi wateja wetu wote kutokana na usumbufu wa kukosa mawasiliano uliosababishwa na kuungua kwa vifaa muhimu vya kuendesha mitambo yetu. Ninaomba niwahakikishie wateja wetu kwamba watarejeshewa huduma zote za vifurushi walizokuwa wamezinunua hapo jana pasipo kutakiwa kuzinunua upya pindi tutakapofanikiwa kurudisha huduma zote za kawaida." Aidha, ninapenda kuwahakikishia kwamba wataalam wetu wanafanya kila jitihada kurudisha mawasiliano ya mtandao wa Vodacom haraka iwezekanavyo," -Mutagahywa.
Posted on: Sat, 17 Aug 2013 07:48:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015