TAKWIMU WINGI WA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA Rekodi zinaonesha - TopicsExpress



          

TAKWIMU WINGI WA MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA Rekodi zinaonesha kuwa Dar Young Africans a.k.a Yanga inaongoza kuwa na mashabiki wengi zaidi kiujumla (yaani ndani na nje ya nchi) ambapo kwa Tanzania pekee kati ya wapenzi wa soka wote nchini mashabiki wa Yanga ni asilimia 63% ikifuatiwa na simba yenye asilimia 35%. Idadi hii kubwa ya Watanzania kuipenda Yanga imeelezwa kuchangiwa zaidi na historia ya nchi pande zote mbili za Muungano, ambapo Yanga iliyoasisiwa mwaka 1935 ilitumika sana kuwakusanya vijana wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika na pia wa Zanzibar, hivyo kujijengea mtandao mkubwa bara na visiwani. Simba kwa upande wake jina lake hili la Simba liliasisiwa rasmi mwaka 1972 yaani miaka 11 baada ya uhuru baada ya kushauriwa na mlezi wa Yaga Rais Abeid Amani Karume wabadilishe jina kutoka Sunderland lililokuwa linaonekana kukumbatia ukoloni. Kabla ya Sundeland pia simba iliitwa Queens iliyoanzishwa mwaka 1938. Hali hii ndiyo ilisababisha kwa kiasi kikubwa Watanganyika walio wengi kuiona Yanga kama timu ya wananchi wote na hivyo kuwa na wapenzi wengi nchi nzima. Hii pia ndiyo ilifanya hadi leo hii Yanga kuitwa timu ya wananchi. Yanga pia inaongoza kupendwa nje ya nchi ambapo ina idadi kubwa ya mashabiki katika nchi za DRC, Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi, Msumbiji, Ethiopia, Malawi, Ghana, Zambia, South Africa, Visiwa na Comoro na Seyhelles, na maeneo mengine duniani.
Posted on: Wed, 23 Oct 2013 15:16:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015