...TANZANIA, THE AFRICAN PEARL-THE-NEW PEARL OF THE - TopicsExpress



          

...TANZANIA, THE AFRICAN PEARL-THE-NEW PEARL OF THE WORLD... Ndiyo, ni LULU ya DUNIA hasa, kwa sababu; 1. Ina “MADINI” balaa - hebu wazia GESI ASILIA – kitu Mnazi bay na SONGAS... gas ya Mtwara, Mafia, mwambao wa pwani ya bahari ya hindi n.k 2. Fikiria hasa “URANIUM”, ile iliyoweka ukuu na ubeberu wa Marekani taifa kuu wakati wa vita ya II ya Dunia (WWII) kupitia Albert Einstein (mwanafizikia) aliyetengeneza BOMU balaa kwa kurutubisha viini vya Uranium; madini ambayo yanaifanya SOUTH AFRICA kua miongoni mwa mataifa shupavu na yenye kujitosheleza kwa umeme na miundo mbinu barani Africa, madini ambayo leo Korea ya Kaskazini na Syria ndio hasa “tug of War – Headline ya World Politics na ni Agenda inafanya Marekani inashindwa kusinzia. Sasa kwetu hapa magwiji wa miamba na madini hayo wanasema kuna mamilioni ya hekta katika misitu ya Dodoma ambyo ina hii “dili” pamoja na huko baharini kati ya Zanzibar na Tanganyika. 3. Achana na hayo, bidhaa adimu na ambayo ndiyo ilikua chanzo cha teknolojia ya usafiri wa reli na maji enzi hizooooo za Dunia changa na ugunduzi, MAKAA YA MAWE. Yapo kibao huko kusini mwa nchi na katika Bahari kuu ya Tanzania ndiyo usiseme, mambo manene yamejazana 4. Chukulia kwa undani suala la CHEAP LABOUR inayopatikana hapa bongo. Unamuajiri mtu mgodini na kumlipa kiduuchu and nobody cares, hata serikali sometime pa1 na kwamba watu hawa wanafanya kazi ktk mazingira magum sana.... wajanja wanalijua hili ndiyo maana wanakimbilia huki kila cku. 5. Dili jingine ni urahisi wa kuwekeza hapa, no objection... kodi hakuna kwa miaka mitano, mrahaba (taxable earning) ni 3% baada ya kutoa ghrarama zako zote. So wanakatwa katika faida ya mwisho kabisa na nadhani hata ikiangaliwa vema basi huo mrahaba utakua ni chini ya asilimia 2, (ask economists). 6. Sasa ndo wanapaki mabegi “jamaa” waje, ndani ya Boeing 747-200B-the Air Force One, wapo na ramani nzima ya tanzania na miamba yake.... 7. Hakuna sharti la kuajiri wataalam kidogo tulio nao hapa, jamaa wanakuja na watu ambao unakuta wana uzoefu tu wa kazi na elimu zao za kawaida, wanakuja km “expatriate workers.” 8. Na....................... BAADA YA HAYO, Sasa ndiyo ujiulize kuhusu ujio wa Marekani na Wachina kibao hapa bongo. Kulingana na mitandao na vyombo vya habari, kwa wale wanaockiliza, hakuna Rais wa Marekani aliyewahi kutumia zaidi ya siku tatu akiwa katika nchi 1 kwenye ziara yake nchi za nje, achilia mbali nchi ya Africa. Last time Pres. Bushi alikuja akakaa siku nne...!!! kwao wakahoji sana. Unajua ni kwanini? Coz mipango nyeti na ya siri hua haisemwi ovyo kwa vyombo vya habari na watu wa kawaida bali kwa wale tu waliokula yamini kufa na kupona na jumuia fulani. So hata Wamarekani wa kawaida hawajui nn kinaendelea ila tu wale magwiji wa uchumi na teknolojia wa serikali na washika biashara ya nchi ambao wanaendesha nchi ya Marekani na uchumi wa Dunia wakishiriakiana na serikali iliyo madarakani. Leo Obama, the genius anakuja na anakaa siku tatu mfululizo, kwao kuna baadhi ya watu wanahoji. Anatia tima na kikosi cha watu mia saba (700). Jiulize, wanakuja kufanya nini???? Kwamba wanaipenda sana Tanzania kwa kua ni Nchi yenye amani na Democrasia hata wakaamua kuja kutalii na kijifunza jinsi tunaendesha mabo haya kwa ufanisi? Eti kwamba tuna tumia vizuri misaada kuliko nchi nyingine ya Africa hata tukawa mfano? Kwa kua hawajui vurugu ambazo zipo na mpige mtoe macho mg’oe kucha au muue ambazo zinaendelea? Kwa kua hawoni jinsi gani viongozi wanakula raha na kutumia rasilimali za nchi vibaya? Kwa kua sio wo au majirani zao walio tuuzia radar na kusema radar ilukua feki hivyo fedha zirudishwe? Sio wao wanaopewa rasilimali kwa misaada ya kutoa neti, salam-kinga, na barabara zinazojengwa ovyo? Mh..... mwenzenu hata sijielewi.... Ninachofahamu ni kua, hiyo team ya wa 700 ina wataalam na ma – analyist nguli na cream ya juu kabisa yenye mchanganyiko wa vinasaba vya kiyahudi kama alivyokua Einstain, na wanakuja kuweka sawa mipango. Halafu, kuna kitu kinaitwa Mkutano wa SMART PARTNASHIP – maraisi na wataalamu wapo wanafanya majadiliano juu ya maendeleo. Baada ya hapo, mkutano mkuubwa kabisa wa wake wa maraisi wanafanya maongezi yao na wao. Habari ndo hiyo. Nashukuru kwa kua tutapata na kauzoefu kidogo, ndugu zetu watapata japo ajira za kuendeshea maisha yao na kusomesha vijana wetu shule. Pia, tutapiga hatua fulani kwenye maendeleo hasa miundo mbinu, ujenzi, umeme na vitu kama hivyo. Nahisi itakuja zama kua Tanzania itagwanywa kwa kanda kulingana na interest za wawekezaji.... .......nadhani, MGENI NJOO MWENYEJI APONE.... I am OPTIMISTIC.........
Posted on: Sun, 30 Jun 2013 08:41:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015