TIMU YA TAIFA YA BURUNDI YAFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA AFRIKA. Timu - TopicsExpress



          

TIMU YA TAIFA YA BURUNDI YAFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA AFRIKA. Timu ya Taifa ya Burundi ijulikanayo kwa jina la Intamba Murugamba imefuzu nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Afrika la wachezaji wanochezea Ligi za ndani. Mchezo huo ulianza kwa kuchelewa kidogo kutokana na swaumu ya ramadhani,kipindi cha kwanza kilimaliza kwa sare ya bao 1-1, timu ya Sudani ndiyo iliyoanza kuliona lango la Burundi kabla ya Burundi kurejesha bao hilo kupitia mchezaji wake machachari tambwe khamisi, mpaka mpira unakwisha Burundi 1-1 Sudani.ikumbukwe kuwa mchezo wa awali uliochezwa mjini bujumbura ulimalizika sare ya bao 1-1 hali iliyopelekea kupiga mikwaju ya penalty na hatimae timu ya Burundi kuibuka mshindi 4-3, kwa matokeo hayo Timu ya Burundi itajiunga na timu zengine ambazo zimefaulu kushikiri katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika nchini Afrika kusini hapo mwakani. Wakati timu ya Burundi (intamba murugamba) inasherekea kwa kufuzu huku timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imetolewa katika mashindano hayo kwa kushushiwa mvua ya magori na timu ya Uganda.
Posted on: Mon, 29 Jul 2013 20:54:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015