TOA MAONI YAKO:- Sehemu ya 18 ya Simulizi ya UGALI DAGAA - TopicsExpress



          

TOA MAONI YAKO:- Sehemu ya 18 ya Simulizi ya UGALI DAGAA ikisimuliwa wa Mtangazaji wako CHRIS BEE... Usikose kusikiliza kuanzia saa 4:20 Usiku..... Baada ya kupita siku mbili nikimaanisha Siku ya Ijumaa NYATONYATO akaamua kwenda msikitini kuswali na USTADHI ISSA ndiye alikuwa akiendesha Ibada….. USTADHI ISSA:- alikuwa akiwaasa vijana kutokata tama na kumtanguliza mwenyezi Mungu…. Na akatolea mfano wa aya isemwayo…. Kubashiriwa Pepo kwa Mtume Muhammad hakukumfanya asitishe Ibada, urafiki wa Ibrahim na Allah haukumfanya awe na kiburi. Baada ya Swala kuisha NYATONYATO akawa anarudi nyumbani kwa wazazi wake na kukutana na SALEHE KAUZIBE ambaye ni rafiki yake mkubwa aliyeamua kumzunguka na kumtongoza MISS MIYEYUSHO ambaye ni Mpenzi wa NYATONYATO na maneno haya ndiyo SINAHELA HAZIMTOSHI aliwahi kumtamkia MISS MIYEYUSHO Kwanza hana mbele wala nyuma juu ya maisha yako wewe kula, kulala unawategemea wazazi. Pili:- elimu yako haijakukomboa unashindwa kuwa mpembuzi wa faida na hasara ya kuoa bali unakurupuka kuoa wakati hujajipanga. Tatu:- eti yeye ni mwanaume wa shoka nikitaka pesa yoyote ya matanuzi, na nikitaka kupelekwa popote hata iwe Ulaya yeye uwezo anao na endapo nikimkubalia leo leo ananipeleka kwa wazazi wake. Nne:- kuwa na wewe napoteza muda isitoshe hatufahamiani kiundani zaidi wewe unalengo la kutimiza haja zako na kuondoka. ...... Baada ya NYATONYATO kuambiwa hivyo alishtuka sana na alionekana ni mtu ambaye kama kaharibiwa siku na kuwa na simanzi sana,…………. Burudani – Jaguar Kigeugeu Baada ya kukutana uso kwa uso NYATONYATO na rafiki yake SALEHE KAUZIBE …… NYATONYATO alishtuka sana na kujikuta akitamani kutamka neno kuwa safari hii ndugu yangu tunakoelekea sasa ama hakika mimi na wewe tutaonana wabaya….. SALEHE KAUZIBE:- Duuuh kulikoni kaka mkuu daaah lawama tena bila salamu….. Asalaam Wallekum…? NYATONYATO:- Wallekum msalaamu….. Kaifa. SALEHE KAUZIBE:- Twahibu,…….. Hajambo Shemeji? NYATONYATO:- Poa, Ujue hakuna mtu aliyewahi kusafiri safari iitwayo maisha, bila kupitia matatizo, kuna kushindwa, kukata tama na hatimaye mafanikio na unifanyialo leo nawe mbeleni litakutokea na kwanini kuvunjiana heshima kama marafiki, tena ndugu tunaofahamiana SALEHE KAUZIBE na iweje tena kuniharibia na kipi unachokitaka kutoka kwa mpenzi wangu MISS MIYEYUSHO wakati awali ulishasema najitishwa zigo la misumari ya kuwa hajatulia ana tabia chafu ni bingwa wa viduku na vigodoro?........ Tutaonana wabaya - QCHILLAH SALEHE KAUZIBE:- ha ha ha ha kaka mimi na wewe ni maswahiba wakubwa mno…. usinisingizie mimi si mhuni ufikiriavyo, mbona hujiamini, siwezi kumchukua MISS MIYEYUSHO kwasababu mimi na mpenzi wangu, na namheshimu kama shemeji yangu tena kwangu yeye ni rafiki tu kaka. NYATONYATO:- SALEHE KAUZIBE kuna usemi usemao vuta ni kuvute kila mtu huvutia kwake, ila nduguyo anapofanikiwa usimwekee kivuli cha kinyongo kwa maana Allah hugawa riziki kwa muja wake badala yake piga moyo konde mafanikio huja kama ndoto. Pesa zako isiwe sababu ya kunivurugia penzi langu tambua nampenda sana MISS MIYEYUSHO…… Shababi – Ally KIba ft Marlaw & Geez Mabovu… Wakati hayo yote yakitokea MAMA PEKUPEKU kutokana na kuwekwa Kitimoto na umoja wa akina mama huko Kijijini Ikuti kwa Jazba mara baada ya kurudi nyumbani akamwita na kuzungumza na mwanae…. MISS MIYEYUSHO:- Abee mama……. MAMA PEKUPEKU:- Mwanangu dunia ni tambala bovu na Mungu hajatuahidi safari rahisi ya maisha ila katuahidi kufika Salama kama vile kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe, kuishi katika imani na upendo, haupaswi kuteteleka usirudi nyuma mpendwa mwanangu mbele kuna mafanikio na ushindi. MISS MIYEYUSHO:- Asante sana mama, unajua wewe ni msingi mzuri katika maisha yangu lakini mbona leo wanipa maneno yenye Baraka na wakati hukuwa na utaratibu huo? Toa maoni yako,,,,,,#### 1. Unadhani NYATONYATO alipaswa kuchukua uamuzi gani na unamshauri nini? 2. Je unamshauri nini MISS MIYEYUSHO na MAMA PEKUPEKO Wafanye nini? 3. Wazazi wa MISS MIYEYUSHO wanapaswa kuchukua uamuzi upi? 4. Ungekuwa wewe ungefanyaje?
Posted on: Wed, 21 Aug 2013 19:27:08 +0000

Trending Topics




© 2015