TOKA CHARANGA MPAKA MTANDIO NDEMBENDEMBE. Mwanzoni mwa miaka ya - TopicsExpress



          

TOKA CHARANGA MPAKA MTANDIO NDEMBENDEMBE. Mwanzoni mwa miaka ya tisini kitenge kilikuwa juu,huu ndio wakati urafiki,Mwatex na Musoma textiles walichanua kibiashara, kila mahali nilipopita watu walikuwa ndani ya vitenge,mashati ya vitenge,sketi za vitenge mpaka suti na kofia, Khanga pia zilikuwepo,tena zenye maandishi yanayovutia kama "TANZANIA AMANI DAIMA,TUULINDE MUUNGANO, ASANTE MUNGU, TENDA WEMA UENDE ZAKO,MAMA NI MAMA n.k!, Kisha ikaja awamu ya mapinduzi ya khanga,awamu ya Majungu na vijembe,ndipo zikaja hizi "SIMUACHI HATA MKILOGA,NAJIAMINI NIMEJAALIWA,UKIONA CHA NINI WENZAKO TUTAKIPATA LINI,RIZIKI KWA MAFUNGU,SIRI YA MTUNGI SHAHIDI KATA n.k" Mh hapa wataalam wakaona bado na kuamua kulitambulisha rasmi vazi la Charanga(hii ilikuwa ni sketi ndefu ya Marinda), hii ikavuma kwa muda kabla wadau hawajaanza na sketi Mpasuo,mpasuo mmoja na baadae mipasuo miwili. Mwishoni mwa miaka ya tisini akaibuka mdudu "KITOPU" naye akaenea kwa kasi kwa wito mkuu wa wadau,ndipo tukaanza kushuhudia suruwali bana misuli mpaka tukazoea hali hiyo. Sasa katika kufanikisha zoezi la kumkufuru Mungu aliyewaumba baadhi ya wanawake wa kisasa wamepiga hatua kubwa, Mwanamke anaweza kuchukua hata masaa 3 chumbani akijiremba na kuvaa, lakini ajabu bado atatoka nje uchi akiwa kajifunika na vitambaa vichache vya nguo,achilia mbali hivyo vitambaa sasa wanavaa mpaka kamba! sasa jiulize alikuwa anavaa au anavua?, wakati wewe ukidhani watu huvaa nguo watokeze hadharani basi wadada wengi wa sasa huvua nguo watokeze hadharani. Tunaamini kwamba Hijab ndilo vazi lenye heshima na kumsitiri mwanamke vema tangu enzi na enzi lakini Hijabu nyingi sasa ziko modified hata kwa baadhi wavaao ninja, hijab nyingi za sasa ni za vitambaa laini sana kiasi cha kuonyesha Maumbile yote ya Muhusika, naye muhusika huyo hata nguo ya ndani havai.je amejisitiri?, zilianza suruwali bwanga,mipasuo, vimini,skin jeans,khanga ndembe ndembe na sasa Mtandio ndembe ndembe na mwisho watatembea wakiwa watupu kabisa kama walivyozaliwa(Uncivilized tena).
Posted on: Tue, 30 Jul 2013 09:57:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015