Togo na Ethiopia wazisaliti timu zao za taifa Shirikisho la - TopicsExpress



          

Togo na Ethiopia wazisaliti timu zao za taifa Shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA imerahisishiwa kazi ya kuzipokonya ushindi timu za taifa za Togo na Ethiopia baada ya nchi hizo zote kukiri kuchezesha wanandinga wasiostahili katika mechi zao za makundi ya bara la Afrika kuwania kucheza fainali za kombe la Dunia za 2014 huko Brazil. Nchi nyingine ambayo ipo mkumbo wa Togo na Ethiopia ni Equatorial Guinea ambayo nayo imeshitakiwa kwa kosa kama hilo na ikipatikana na hatia Kundi B litaathirika hasa Tunisia ambao walikwisha fuzu. Ethiopia ambao walikuwa wameshafuzu kutoka Kundi A wakiwa na Pointi 13 wamekiri kuchezesha mchezaji ambaye hakupaswa kucheza kwenye pambano lao dhidi ya Botswana na hivyo ni wazi FIFA itaipora Pointi 3. Kwa upande wao Togo wamekiri kupitia mjumbe wa Shirikisho lao la Soka Toussa Komi Gabriel kumchezesha Alaixys Romao walipoifunga Cameroun 2-0 mjini Lome Juni 9 huku mchezaji huyo akiwa na kadi za njano mbili. Nao Equatorial Guinea ambao waliwafunga Cape Verde mabao 4-3 wanadaiwa kwenye mchezo huo kumchezesha mchezaji asiestahili. ZILIZOINGIA RAUNDI YA MWISHO YA MTOANO YA TIMU 10: -Ethiopia [KUNDI A] -Tunisia [KUNDI B] -Ivory Coast [KUNDI C] -Egypt [KUNDI G] -Algeria [KUNDI H] ***BADO 5: ZINAWEZA KUWA: -KUNDI D: Ghana au Zambia -KUNDI E: Burkina Faso, Congo au Gabon -KUNDI F: Nigeria au Malawi -KUNDI I: Libya, Cameroun au Congo DR -KUNDI J: Senegal au Uganda Xxxxxxxxx Kituko: Alcantara apeleka ujumbe Barcelona Baada ya pambano la fainali ya U21 kuisha kati ya Hispania na Italia mchezaji wa Hispania na Barcelona Thiago Alcantara alionekana amebeba mpira uliokuwa na maandishi ya Kihispania "Nos Vemos en Manchester" yakiwa na maana "tutakutana Manchester". Taarifa zinasema maneno hayo yameandikwa na mmoja ya wachezaji wa Hispania bila ya kutajwa jina lake lakini ukweli ni kwamba David de Gea ndiye mchezaji pekee wa Man Utd aliyepo kwenye timu hiyo ya Hispania. Thiago amekuwa akihusishwa kuhamia Man Utd lakini klabu yake ya Barcelona bado inamshikilia asiondoke kwa kile kinachosemekana ndiye mrithi wa Xavi na Iniesta. Hadi sasa Thiago mwenyewe ameshaonesha nia ya kuhamia United ili aweze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza tofauti na Barcelona ambapo mara zote anaanzia benchi. Msimu wa usajili bado unaendelea hivyo lolote linaweza kutokea na Thiago akajiunga na United. Thiago alibeba mpira huo ikiwa ni kumbukumbu yake baada ya kufunga magoli matatu kwenye mechi hiyo ya fainali ambapo Hispania iliondoka na ushindi wa magoli 4-2 na kunyakuwa kombe la Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21.
Posted on: Thu, 20 Jun 2013 18:28:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015