Tuanze kujenga utamaduni wa kupeana majukumu ya kitaifa kwa - TopicsExpress



          

Tuanze kujenga utamaduni wa kupeana majukumu ya kitaifa kwa kuujali zaidi utanzania kuliko migawanyiko yetu midogo midogo isiyo na tija kabisa. Tufanye hivi:- Likitokea suala la mgogoro kisheria wa kimataifa kama mgogoro wetu wa mpaka na Malawi, tusiwaache kwenye timu yetu ya kukabili suala hilo kina Professor Costa Mahalu na Tindu Lissu. Linapokuja suala llinalohusu ardhi yetu, wasiwe pembeni kina Dr Ringo Tenga na Professor Mgongo Fimbo. Kwenye masuala ya bishara ya kimataifa na uchumi, tusiwaache kina Professor Ibrahim Lipumba, Dr Cyril Chami, Dr Adolph Mkenda na Mheshimiwa Zitto Kabwe. Kwenye masuala ya uhandisi asiwekwe pembeni Mheshimiwa James Mbatia. Aidha, tusiache vichwa makini vya kutoka Tanzania Visiwani katika maeneo yote hayo.Tuanze utaratibu huo utakaotupatia tija kubwa kama taifa na tujitahidi kuuzoea. Tujiepushe kuogopa kutambiwa kwa upande mmoja na kutamba kwa upande mwingine kwamba "hili lisingefanikiwa bila ya sisi". Utoto huo,kwani ninyi kina nani, si Watanzania? Kwani mmelifanikisha peke yenu? Naomba tusiache raslimali watu yetu bora ikikaa tu wakati tunaweza kuitumia kwa manufaa. Mungu ibariki Tanzania.
Posted on: Mon, 22 Jul 2013 01:58:34 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015