Tuliyokuandalia katika Amka na BBC asubuhi hii .... Nchi tano - TopicsExpress



          

Tuliyokuandalia katika Amka na BBC asubuhi hii .... Nchi tano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa zimekuwa zikiijadili Syria huku kukiwepo taarifa kwamba Urusi imeiwasilishia Marekani mpango wake wa kuzidhibiti kimataifa silaha za kemikali za Syria. Viongozi 160 wa kidini nchini Somalia watoa maamuzi kwa misingi ya dini ya kiislamu, dhidi ya Al Shabab. Utawasikia pia watu wanaodai kuwa raia wa Tanzania ambao wamegoma kwenda Rwanda baada ya kufukuzwa mpakani Rusumo, kwa kutuhumiwa kuwa wahamiaji haramu. Jiunge nami Maryam Dodo Abdalla muda usio mrefu nikupashe kwa kina taarifa hizi miongoni mwa nyengine.
Posted on: Thu, 12 Sep 2013 01:14:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015