UHURU IN NAROK AND KAJIADO… RAIS UHURU KENYATTA AMBAYE - TopicsExpress



          

UHURU IN NAROK AND KAJIADO… RAIS UHURU KENYATTA AMBAYE ANAADHIMISHA MIAKA 52 HII LEO, ANAONGOZA HAFLA YA KUTOA SHUKRANI INAYOANDALIWA KWA NIABA YA WAZIRI WA MASWALA YA NDANI JOSEPH OLE LENKU HUKO LOITOKTOK COUNTY YA KAJIADO.BAADAYE RAIS UHURU AMEPANGIWA KUELEKEA ENEO LA MASAI MARA HUKO NAROK KUFUNGUA RASMI KAMBI YA MAHALIMZURI AMBAYO INAYOMILIKIWA NA WAWEKEZAJI WA UINGEREZA RICHARD BRANSON.RAIS UHURU PIA AMEPANGIWA KUHUDHURIA HALFA YA KUTOA SHUKRANI YA MBUNGE MTEULE JANET TEYAAI HUKO NGONG COUNTY YA KAJIADO. WESTAGATE SUSPECTS MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE KUHUSU ULINZI NDUNGU GITHINJI AMESISITIZA KUWA WASHUKIWA WANNE WA UGAIDI WALIOTEKELEZA SHAMBUALIZI KATIKA JINGO LA WESTGATE WALIWAWA.AKIONGEA KATIKA ENEO BUNGE LAKE LA TETU GITHINJI ANASEMA KINYUME NA MADAI YALIYOTOLEWA MAGAIDI HAO WALIWAWA NA WANGALI WANASUBIRI MATOKEO YA UCHUNGUZI WA KUBAINI ASILI YAO.GITHINJI AMEVITAKA VYOMBO VYA HABARI VILIVYO NA KANDA ZA VIDEO AMBAZO NI MUHIMU KUFUATIA SHAMBULIZI HILO KUWASILISHA KWA SERIKALI KABLA YA KUPEPERUSHWA.AMEONGEZA KUWA WENGI WA VIJANA WAMEKUWA WAKIHADAIWA NA KUJIUNGA NA KUNDI LA AL SHAABAB. CHURCH LEADERS FROM EMBU COUNTY VIONGOZI WA KIDINI KUTOKA KAUNTI YA EMBU WAMEJITENGA NA USEMI ULIOTOLEWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA KIDINI WANAOUNGA MKONO KUTAMBULIWA KWA MASHOGA KANISANI NA KATIKA JAMII.VIONGOI HAO WAKIONGOZWA NA ASKOFU MWITI WANASHIKILIA KUWA BIBILIA INATAMBUA TU NDOA KATI YA MTU WA KIKE NA KIUME.MWITI ANASEMA USHOGA NA USAGAJI HAUKUBALIKI KATIKA JAMII YA KIAFRIKA NA KUWATAKA VIONGOZI HAO KUTOWAPOTOSHA WAKENYA.ANASEMA VIONGOZI WA KIDINI WALIOTOA MATAMSHI HAYO WANA LENGO LA KUPOKEA FEDHA KUTOKA KWA MASHIRIKA YANAYOUNGA MKONO MAHUSIANO HAYO. RUTO COMING… NAIBU RAIS WILLIAM RUTO ANATARAJIWA KUWASILI NCHINI SAA MBILI USIKU WA LEO NA ATAKUWEPO NCHINI KWA SIKU TATU.MAHAKAMA YA ICC ILIMRUHUSU RUTO KUTOHUDHURIA VIKAO VYA KESI DHIDI YAKE KWA SIKU 3.RUTO ANAREJEA NCHINI ILI KUMPA FURSA RAIS UHURU KENYATTA KUELEKEA KIGALI RWANDA KWA MKUTANO WA KIKANDA. LAIKIPIA LAND ROW MZOZO WA ARDHI UNANUKIA KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA KATIKA KIJIJI CHA ERERI KATIKA WILAYA YA LAIKIPIA MASHARIKI HASA KUFUATIA KUTEKETEZWA KWA KITUO CHA POLISI KATIKA ENEO HILO.INAARIFIWA MZOZO HUO UMEIBUKA BAADA YA WAMILIKI WA MASHAMBA KUANZA KUJENGA KATIKA MASHAMBA AMBAYO YAMEKUWA YAKITUMIKA NA WAFUGAJI WA KUHAMA HAMA.WAKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO ULIOONGOZWA NA MWENYEKITI WA TUME YA KITAIFA YA ARDHI MOHAMED SWAZURI WAFUGAJI HAO WANAPINGA KUFURUSHWA KUTOKA ENEO HILO WAKIDAI NI KINYUME NA SHERIA.HATA HIVYO WAMILIKI WA ARDHI HIYO WANASEMA HIYO NI MALI YAO. KIMATAIFA. VIONGOZI WA MATAIFA YA MAGHARIBI MWA AFRIKA WALIANDAA MKUTANO NA KUTOA WITO KWA JAMII YA KIMATAIFA KUINGILIA KATI NA KUREJESHA HALI YA UTULIVU NCHINI MALI.AKIONGEA KATIKA MKUTANO ULIOANDALIWA MJINI DAKAR SENEGAL RAIS WA SENEGAL MACKY SALL ALIMKARIBISHA MWENZAKE IBRAHIM BOUBACAR KEITA NA KUWATAKA VIONGOZI WENGINE KUMUUNGA MKONO KATIKA JUHUDI ZA KULETA AMANI MALI.AMETAKA JAMII YA KMATAIFA KUWATUMA WANAJESHI ZAIDI KUSHIRIKIANA NA WALE WA UMOJA WA MATAIFA WALIOKO KWA SASA.
Posted on: Sat, 26 Oct 2013 13:01:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015