ULINIUA GLORIA 10 Peter alionekana kuwa mwenye hasira kali, - TopicsExpress



          

ULINIUA GLORIA 10 Peter alionekana kuwa mwenye hasira kali, kisu kilikuwa mkononi mwake, kwa wakati huo, kichwa chake kilikuwa kikifikiria kufanya mauaji tu. Moyo wake ukawa umekwishabadili ka kabisa, hakumpenda Gloria, mapenzi yote ambayo alikuwa nayo kwa Gloria yalikuwa yamekwishapotea na ni chuki tu ndio ambazo zilikuwa zimeutawala moyo wake. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kutoka na hasira kali ambazo alikuwa nazo katika kipindi hicho, hakuamini kama msichana Gloria, msichana ambaye alikuwa na pete ya uchumba kidoleni mwake ndiye ambaye alikuwa ameamua kuyafanya yale aliyokuwa ameyafanya. Huku akiwa hatua saba kumfikia Gloria, mlinzi akamuwahi na kisha kumshika. Peter akaanza kuleta purukushani lakini kutokana na kushikwa vilivyo na mlinzi yule, akajikuta akiishiwa nguvu, machozi yaliendelea kumtoka lakini hakuwa na la kufanya. “Nitakuaa....ni mesema nitakuua” Peter alimwambia Gloria kwa sauti kubwa. Mambo yakaonekana kubadilika mahali hapo, alichokifanya Bwana Stewart ni kumchukua Gloria na kisha kumpeleka nje ya jengo lile na kumuingiza garini mwake. Katika kipindi chote hicho Gloria alikuwa akilia kama mtoto, Peter alionekana kubadilika katika mabadiliko ambayo Gloria hakuwa ameyaona kwake katika kipindi chote cha maisha yake. “Kwa nini Peter anataka kukuua tena?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo lilitoka mdomoni mwa Bwana Stewart ambaye alikuwa akiliwasha gari lake. “Sijui kwa nini. Amekuja na kuonekana mwingi wa hasira” Gloria alidanganya huku akilia. “Ndio akuite malaya!” “Hata mimi nimemshangaa sana” “Kwani alikwishawahi kukufunua?” “Kivipi” “Alikwishawahi kufanya mapenzi na wewe?” Bwana Stewart aliuliza huku akiendesha gari. “Peter ni mchumba wangu” Gloria alisema maneno ambayo yakamfanya Bwana Stewart kushtuka na kusimamisha gari lile pembeni ya barabara. “Umesemaje?” “Peter ni mchumba wangu. Hii pete alinivarisha yeye mbele ya wazazi wangu” Gloria alimwambia Bwana Stewart. “Unanichanganya . Kwa hiyo Peter ni Mtanzania kama wewe?” “Ndio” “Na vipi kuhusu Kaposhoo?” “Yule si mpenzi wangu” Gloria alitoa majibu ambayo yalimfanya Bwana Stewart kuchanganyikiwa . “Mbona haukuniambia? Mimi nilijua Kaposhoo ni mpenzi wako kutokana na ukaribu wenu” Bwana Stewart alimwambia Gloria. Hapo ndipo ambapo Gloria akaanza kumhadithia Bwana Stewart toka katika kipindi ambacho Peter alikuwa amemvarisha pete katika sherehe ndogo iliyofanyika nyumbani kwao. Gloria hakuishia hapo, aliendelea kumhadithia mpaka katika kipindi ambacho Peter aliamua kuondoka nchini Tanzania na kuelekea Zambia kwa ajili ya kusoma. Katika kipindi chote hicho Bwana Stewart alikuwa kimya kabisa, kichwa chake kilikuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu. “Kwa hiyo Kaposhoo alikuwa rafiki wa Peter?” Bwana Stewart alimuuliza Gloria. “Ndio” “Kwa hiyo nimeua damu isiyo na hatia?” Bwana Stewart aliuliza. “Kivipi?” “Niliwatuma vijana wamteke Kaposhoo na kumuua. Wamekwishaifany a kazi hiyo” Bwana Stewart alimwambia Gloria. “Umemuua kaposhoo” “Ndio. Mbona umeshtuka sana na wakati tulikuwa tushakubaliana? ” “Usingefanya hivyo” “Sasa haukuniambia mpenzi, unafikiri ningefanyaje” “Ok! Hakuna tatizo” “Ila kuna kitu nimefikiria” “Kitu gani?” “Kwanza futa machozi, sipendi kuyaona machozi yako yakitiririka mashavuni mwako” Bwana Stewart alimwambia Gloria ambaye akaanza kuyafuta machozi yake. “Bado kuna kizingiti kikubwa mbele yetu” Bwana Stewart alimwambia Gloria. “Kizingiti gani?” “Peter. Anaweza kukua huyu mtu” “Hawezi kuniua” “Hawezi! Haujaona pale alivyotaka kukuchoma kisu, hivi yule mlinzi asingemuwahi si ungekuwa marehemu pale” “Kwani si hata wewe ungemzuia” “Na uzee wangu huu, si angeniua hata kwa ngumi moja” “Ok! Baby, wewe unataka nini kifanyike?” “Tumuue Peter ili tuwe na amani. Tusipomuua, atakuua yeye” Bwana Stewart alimwambia Gloria. “Mmmh!” “Usigune. Hilo ndio la msingi” “Tutaanzia wapi?” “Hilo si swali la kujiuliza sana, cha msingi ni utayari tu. Upo tayari” Bwana Stewart alimwambia Gloria na kisha kumuuliza swali. “Kwa sababu anataka kuniua, nipo tayari” Gloria alimwambia bwana Stewart. “Basi hakuna tatizo” Huo ndio mpango ambao walikuwa wameufikiria kufanyika katika kipindi hicho. Kwa sababu tayari Peter alionekana kuwa mtu mbaya ambaye angeweza kuweka kizingiti katika mahusiano yao basi nae alitakiwa kufa kama alivyokufa Kaposhoo. Kwa wakati huo, Gloria hakuonekana kuwa na roho ya huruma hata mara moja, kitu alichokiona cha kumuua Peter kwake kilikuwa sawa kabisa, hakujisikia huruma yoyote moyoni mwake, kumuua Peter kwa ajili ya kulilinda penzi lake na mtu aliyekuwa na umri kama wa baba yake kilionekana kuwa sahihi kabisa. Bwana Stewart akaonekana kuridhika, kitendo cha Gloria kukubali kumuua Peter kilionekana kumpa furaha sana, alijiona kuwa stering ambaye alikuwa akifanya kila kitu ambacho alitaka kukifanya kwa wakati huo. Hakutaka mtu yeyote aingilie mahusiano yake na Gloria, alimpeda sana Gloria, kwake, alionekana kuwa msichana mrembo sana ambaye hakutakiwa kumpoteza hata mara moja. Suala la kumuua Peter wala halikuwa kubwa kabisa, tukio hilo alilifananisha na kumsukuma mlevi katika mteremko mkali. Kufanya mauaji kwa ajili ya kulilinda penzi lake hakukuonekana kama kulikuwa na kosa lolote lile, alikuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote kile kwa ajili ya kuliokoa penzi lake kwa Gloria. “Ngoja nifanye mipango, kesho tu utasikia taarifa kwamba huyu mtu ni marehemu” Bwana Stewart alimwambia Gloria. “Utafanyaje?” “Kama Kaposhoo alivyouawa. Usijali mpenzi” Bwana Stewart alimwambia Gloria. Kilichoamuliwa ndicho ambacho kilitakiwakufan yika, alichokifanya Bwana Stewart ni kuwafuata vijana wa kundi la Kunta Kinte na kisha kuwaambia juu ya mpango wake kabambe ambao alikuwa ameuweka kwa ajili ya kumuua Peter. Mpango huo ukapokelewa kwa mikono miwili na aliahidiwa kwamba ndani ya siku mbili tu kila kitu kingekuwa tayari endapo angewakabidhi picha ya marehemu mtarajiwa. “Wanahitaji picha yake” Bwana Stewart alimwambia Gloria. “Nafikiri ninazo kwenye simu. Subiri” Gloria alimwambia bwana Stewart na kisha kuanza kuipekua simu yake ambapo mara baada ya kuziona picha kadhaa za Peter, akampa Bwana Kaposhoo. Siku iliyofuata, Bwana Stewart akaanza kuelekea katika makao makuu ya kundi la Kunta Kinte na kisha kuwapa picha zile. Kila kitu ambacho kilitakiwa kukamilishwa hasa kuhusiana na alipo kikakamilishwa na kisha kupewa ahadi kwamba baada ya siku mbili kazi yake ingekamilika kwani kamwe hawakuwa wameshindwa katika kazi yoyote ile hasa ya kufanya mauaji. “Kama ilivyotokea kwa Kaposhoo, itatokea kwa huyu mjinga pia. Atamiminiwa risasi nyingi tu” Kiongozi wa kundi lile alimwambia Bwana Stewart. “Kwa hiyo ndani ya siku ngapi itakuwa tayari?” “Leo usiku tutakupigia simu ya ushindi. Kazi itafanyika leo usiku” Kiongozi yule alijibu kwa kujiamini. “Itakuwa safi sana” Bwana Stewart hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, kwa kuwa alikuwa amekwishafanya kila kitu kuhusu malipo, akaondoka mahali hapo na kurudi nyumbani. Ndani ya gari alikuwa na furaha kwa kuona kwamba kila kitu ambacho alikuwa amekipanga kilikuwa kikienda kukamilika muda si mrefu. Moyoni hakujua, hakujua kwamba unapoingia ndani ya vita kupigana na adui yako huku ukimuwinda na risasi nawe pia unawindwa na adui huyo. Hayo ndio yalikuwa maisha yaliyoanza kutokea, wakati yeye akimuwinda adui yake, nae huku nyuma alikuwa akiwindwa pia. Je nini kitaendelea? Je Bwana Stewart ataweza kukamilisha mipango yake?
Posted on: Sat, 03 Aug 2013 08:30:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015