UONGOZI WA KIJIJI CHITA KUKUTANA NA TANESCO KILOMBERO Jengo la - TopicsExpress



          

UONGOZI WA KIJIJI CHITA KUKUTANA NA TANESCO KILOMBERO Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Melela kata ya Chita Wilayani kilombero limekamilika na bado kupauliwa. Akiongea na Pambazuko Fm Mjini Ifakara alasiri ya Leo Diwani wa Kata ya Chita Bwana Hassan Kidampa amesema kuwa siku saba walizoahidi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala zimekwisha na tayari wamekamilisha na yupo Mjini Ifakara kwa ajili ya Kufuatilia Fedha Milioni 30 kwa ajili ya kupaulia na kukamiliasha jingo hilo. Bwana Kidampa amesema kuwa kutokana na ushirikiano na Uongozi uliopo na Wananchi kumepeleka kukamilishawa haraka aahadi yao. Alipoulizwa juu ya kupatikana kwa Mtendaji wa zamani wa Kijiji cha Chita Bwana Litauna Litaunga aliyekuwa anatafutwa na Serikali amesema kuwa suala hilo lipo Mikononi mwa Jeshi la Polisi na kwamba amesikia taarifa za Bwana Litaunga kwenda kuripoti Kituo cha Polisi Mngeta. Kuhusu suala la Maandamano ya Wananchi wa Chita wakidai Wapatiwe Umeme na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bwana Kidampa amesema kuwa amekaa na wananchi wa Kijiji hicho na kuwaeleza walipofikia juu ya suala hilo huku Uongozi wa Kijiji upo njiani kuitisha kikao na TANESCO kwa ajili ya Majadiliano yatakayofanyika Katika Mgodi wa Kihansi uliopo Takribani Kilomita 15 kutoka Kijijini hapo. Kijiji cha Chita kilichopo Kilomita Takribani 15 kutoka Mgodi wa Kuzalisha Umeme wa Kihansi hakina Umeme lakini wananchi wamekuwa wakishiriki kulinda nguzo na miundombinu ya Umeme unaopita kijijijini hapo kwenda meneo mengine ya Wilaya na Mikoani.
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 18:43:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015