Ukumbusho Wa Swawm Ya Aashuraa Alkhamiys 10 Muharram 1435H = 14 - TopicsExpress



          

Ukumbusho Wa Swawm Ya Aashuraa Alkhamiys 10 Muharram 1435H = 14 Novemba 2013M Assalaamu ‘Alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh Tunapenda kuwakumbusha kuhusu Swawm ya ‘Aashuraa ambayo itakuwa Alkhamiys 10 Muharram 1435H (14 Novemba 2013M). Ni vizuri mtu kufunga siku ya kabla yake vilevile ambayo ni Jumatano 9 Muharram na asipojaaliwa basi anaweza kufunga na siku ya baada yake ambayo ni Ijumaa 11 Muharram, na ikiwa ameshindwa basi muhimu hiyo siku ya Alkhamiys 10 Muharram ajitahidi asiikose. 09 Muharram 1435H = Jumatano 13 Novemba 2013M. 10 Muharram 1435H = Alkhamiys 14 Novemba 2013M. Fadhila Za Swawm Ya ‘Aashuraa قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( صيام يوم عاشوراء ، إني أحتسب على الله أن يكفر السنة التي قبله)) رواه مسلم Kasema Mtume (Swalla Allahu alayhi wa aalihi wa sallam): ((Funga ya siku ya Aashuraa, nataraji kutoka kwa Allaah Ayafute madhambi ya mwaka uliotangulia)) [Muslim] Fadhila Za Mwezi Huu Khaswa Ingawa miezi minne yote iliyotajwa katika Aayah ya juu ni mitukufu lakini mwezi huu wa Muharram umefadhilishwa zaidi ya miezi mingine kama ilivyo katika Hadiyth zifuatazo: عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَفْضَلُ الصِّيَامِ بَعْدَ رَمَضَانَ شَهْرُ اللَّهِ الْمُحَرَّمُ )) رواه مسلم Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu anhu) kasema; Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Funga bora kabisa baada ya Ramadhaan ni funga ya mwezi wa Allaah wa Muharram)) [Muslim] عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلّا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَنِان رواه البخاري Imepokelewa na Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu anhuma) ambaye amesema: Sijapata kumuona Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) akisubiri kufunga siku yoyote kama siku hii ya siku ya Aashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhaan [Al-Bukhaariy] Swawm ya Aashuraa imependezeshwa hata kwa watoto kuifunga kama walivyokuwa wakifanya Maswahaba katika siku hiyo. عن الرُّبيّع بنت معوذ رضي الله عنها قالت: أرسل رسول الله صلى الله عليه وسلم غداة عاشوراء إلى قرى الأنصار من أصبح مفطرا فليتم بقية يومه ومن أصبح صائما فليصم ، قالت : فكنا نصومه بعد ونصوّمه صبياننا ... رواه البخاري ومسلم Kutoka kwa Ar-Rubayi bint Muawwadh (Radhiya Allaahu anhaa) amesema: Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alituma ujumbe Alfajiri ya siku ya Aashuraa katika vijiji vya Answaar Aliyeamka akiwa amefuturu amalize siku yake (kwa kutokula) na aliyeamka amefunga afunge Akasema (Ar-Rubayi: Tulikuwa tukifunga baada yake na tukiwafungisha watoto wetu... [Al-Bukhaariy na Muslim] Sababu Ya Kufunga Siku Ya Aashuraa عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: ((مَا هَذَا)) قَالُوا هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ هَذَا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى، قَالَ: (( فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ)) فَصَامَهُ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ رواه البخاري Imepokelewa na Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu anhuma) kasema: Alielekea Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga siku ya Aashuraa, akasema: ((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa Wana wa Israili kutokana na adui wao, na Muusa alifunga siku hii. Akasema (Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mimi nina haki zaidi juu ya Muwsaa kuliko nyinyi)). Akafunga siku hiyo na akaamrisha ifungwe [Al-Bukhaariy] Lakini Mtume wetu (Swalla Allahu alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kuwa tukhitilafiane na Mayahudi kufunga siku hiyo kwa kuongeza siku moja kabla. روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ ا[truncated by WhatsApp
Posted on: Tue, 12 Nov 2013 11:00:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015