Vijana na Siasa Vijana tusidanganywe na vyama vinavyojipambanua - TopicsExpress



          

Vijana na Siasa Vijana tusidanganywe na vyama vinavyojipambanua kuwa ni vyama vya siasa vyenye lengo la kuwakomboa Vijana na watanzania kwa ujumla, ni lazima tuvichunguze kwa kina na kwa kujiridhisha kama ni kweli vina dhamira ya dhati katika yale wanayoyasema, angalia mfano huu wa ZZT ni somo tosha kwa vijana wa kitanzania, alitoka chuoni akakipigania kwa hali na mali akawashawishi vijana wa vyuoni kukisapoti chama 2010 vijana wengi walihamasika na chadema lakini yaliyomkuta Mkosamali mbunge wa muhambwe kwa tiketi ya Nccr, kafulila mbunge wa kigoma kusini kwa tiketi ya Nccr ni ushahidi tosha kuwa chadema hakikuwa na dhamira ya dhati kwa vijana lakini kwa kutambua hivyo vijana hao hawakuchelewa na haraka walijiunga na Nccr mageuzi na kwa kuwa wananchi waliwaelewa waliwapa kura na leo ni wabunge.chadema kipo kwenye ushindani wa kisiasa lakini linapokuja kuwa gumu kwao ni pale viongozi wenye uwezo wakitaka kuchukuwa nafasi muhimu kwenye chama hicho ni lazima wapate dhoruba kali kwa kupoteza maisha yao mf.Chacha Wangwe n.k sasa hadithi hii imemgeukia Zitto kabwe baada ya kosakosa nyingi hatimae avuliwa nafasi zake zoote na kuonekana ni msaliti kwa chama, chama alichokitangaza kwa nguvu kubwa yoote hii ni kwasababu aliutaka Uenyekiti wa chama, laiti dhamira yake isingekuwa kuutaka Uenyekiti leo hii asingekuwa tatizo chadema.Pole Zitto lakini ni fundisho kwa vijana wa kitanzania wenye lengo la kuja kuwa viongozi siku zijazo msikatishwe tamaa na siasa za majitaka zinazoendeshwa na Mze Mtei ndani ya chadema, kwa chama kuendeshwa kwa misingi ya kifamilia. jumapili njema ndugu zangu.
Posted on: Sun, 24 Nov 2013 08:39:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015