Viongozi wa makanisa nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta - TopicsExpress



          

Viongozi wa makanisa nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoshirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi. Wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la AIPCK, Mugecha Karume, viongozi hao wa makanisa wamesema kuwa, kesi hiyo ina mambo mengi yasiyoeleweka na kwa mantiki hiyo, hakuna haja Rais Kenyatta kwenda Hague kwa ajili ya kesi dhidi yake mbele ya mahakama hiyo. Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya Wakenya 1000 waliuawa. Kwa sasa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na Joshua Sang wako mjini Hague ambako kesi zao zinaendelea. Kesi ya Rais Kenyatta inatarajiwa kunza mwezi ujao wa Novemba. Umoja wa Afrika AU pia umetaka kesi hizo zisimamishwe au kuhamishiwa jijini Nairobi ili zisikizwe na mahakama za Kenya.
Posted on: Tue, 08 Oct 2013 09:27:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015