WABUNGE WA ZANZIBAR WAPOKEEA MISAADA YA FUTARI KWA KAMPUNI YA - TopicsExpress



          

WABUNGE WA ZANZIBAR WAPOKEEA MISAADA YA FUTARI KWA KAMPUNI YA KONYAGI Wabunge wa majimbo ya Gando na Ziwani (wote kutoka chama cha CUF) ndugu khalifa Khalifa na Ahmed Nqwali wamepokea msaada wenye thamani ya sh. milioni 8 kutoka kampuni ya Tanzania Distilleries LTD jijini Daresalam, ambayo ndio kampuni inayotengeneza pombe aina ya konyagi. Msaada huo unajumuisha mchele, sukari, mafuta ya kupikia na mbuzi. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, ndugu David Mgwasa amesema msaada huo hutolewa hasa siku za ramadhani ili kuwafanya mayatima walioondokewa na wazazi wao kutokana na ajali ya mv spice na skagit ili wapate kufarijika. Hapa ikumbukwe kuwa, kunasibishwa kwa utoaji wa msaada huo na kampuni ya kutengenezea pombe ni kinyume cha maadili na hakikubaliki, kwani Allah (SWT) ameutaja ulevi kuwa ni vitendo vya kishetani na kututaka tujiepusha navyo. Tunawanasihi wananchi wa majimbo hayo au mengineyo ambayo wataletewa msaada huo kuukataa pamoja na kuwakataa watakaoulpeleta ili kujiepusha na ghadhabu za Mwenyezi Mungu. Kilichozalishwa kwa haramu hakitaleta msaada wala manufaa bali ni maangamizi na adhabu kali kutoka kwa muumba.
Posted on: Mon, 08 Jul 2013 21:06:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015