WACHEZAJI WANAOJIRUSHA WANASTAHILI KUPEWA KADI NYEKUNDI YA MOJA - TopicsExpress



          

WACHEZAJI WANAOJIRUSHA WANASTAHILI KUPEWA KADI NYEKUNDI YA MOJA KWA MOJA. MWENYEKITI wa klabu ya Crystal Palace, Steve Parish ametaka wachezaji wanaojirusha kuonyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja badala ya kadi ya njano kama ilivyo hivi sasa. Kauli ya bosi huyo imekuja kufuatia Ashley Young wa Manchester United kupewa kadi ya njano kwa kujirusha baada ya kugongana na Kagisho Dikgacoi wa Palace katika mchezo baina ya timu hizo iliyochezwa Jumamosi. Dikgacoi alitolewa baadae kwa kadi nyekundu baada ya kugongana tena na Young katika mchezo huo ambao United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Parish amesema kama beki akimzuia mshambuliaji aliyekuwa katika nafasi ya kufunga anapewa kadi nyekundu ya moja kwa moja haoni sababu ya kwanini wachezaji wanaojirusha ili kutengeneza nafasi za kufunga nao kupewa kadi nyekundu pia. Katika mchezo huo mwamuzi Jon Moss alimpa kadi ya njano Young kwa kujirusha katika tukio la kwanza lakini baadae mwamuzi alitoa penati kwa wenyeji kwa faulo aliyofanyiwa Young na Dikgacoi ambaye alipewa kadi nyekundu. Young amekuwa akilalamikiwa hata na makocha wake kwa tabia yake ya kujirusha ambapo kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson aliwahi kusema kuwa mchezaji huyo anaanguka kirahisi sana.
Posted on: Mon, 16 Sep 2013 11:22:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015