WAHANGA WA MADAWA YA KULEVYA KWENDA MAHAKAMANI KULAZIMISHA RAIS - TopicsExpress



          

WAHANGA WA MADAWA YA KULEVYA KWENDA MAHAKAMANI KULAZIMISHA RAIS KIKWETE KUTOA MAJINA YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA AMBAYO YAMESABABISHA VIFO VYA WATOTO WAO NA WENGINE KUWA MAZEZETA. Wahanga wa watoto walikufa kwa sababu ya madawa ya kulevya wanajiandaa kwenda mahakamani baada ya sikuku ya idd ili mahakama kumlazimisha Rais kikwete kutoa na kutaja hadharani majina ya aliyopewa ya vigogo wanauza madawa ya kulevya madawa ambayo yamesababisha vifo na uzezeta kwa watoto wao. Rais Jakaya Kikwete akidaiwa kukalia orodha ya mtandao wa vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya bila sababu yoyote kitu ambacho kinatia shaka wa nini anaendelea kuyakalia na hali madawa ya kulevya yanazidi kuuwa vijana ambao ni taifa la kesho, itakumbukwa takriban miaka saba iliyopita (Septemba 18, 2006), alikabidhiwa orodha ndefu yenye majina 58 yenye majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Orodha hiyo ilijumuisha majina ya wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi wa dini, sambamba na mbinu wanazotumia kufanikisha biashara hiyo haramu. Kwa mujibu wa maelezo husika, kundi la kwanza lilikuwa na majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya viongozi wa dini. Katika kundi la pili kulikuwa na watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa, wamo kutoka taasisi ya fedha na wafanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam na Zanzibar. Kundi la tatu lilikuwa na majina 27 ya watu ambao si wenye majina makubwa lakini ndio waliokuwa wakitumika kusambaza mitaani dawa hizo za kulevya. Unajuwa ndugu mwandishi...........Muuza ‘unga’ hana tofauti na gaidi au mtu anayeambukiza Ukimwi kwa makusudi, wote wauaji. Tukiwaruhusu wanaharamu hawa waendelee na biashara hiyo kana kwamba ni chanzo halali cha kipato, hatima ya taifa itakuwa shakani, ni lazima twende mahakamani hata kama ni yeye anawatewuwa kushika nyizifa hizo labda atanaona watanzania tuko serious na swala hili, lengo letu tunataka Tanzania ambayo ni drug free alimaza mzazi huyo ambaye amepoteza vijana wawili kwa sababu ya madawa ya kulevya ndugu Sumari Ally Kizito. Gazeti hili lilipomtafuta mkuu wa polisi kitengo cha madawa ya kulevya kuhusiana na majina ya vigogo alisema “Wakati mwingine tunasema tu, kama tuna ushahidi kuhusu hilo kwamba rais alipewa majina utolewe. Mimi nalisikia maneno hayo majina ya vigogo wauza madawa ya kulevya lakini sijawahi kuletewa hapa,” Ndugu mwandishi kama unayo nipe sasa hivi utaona kama sitayafanyia kazi, alijigamba kamanda huyo wa polisi mwenye sifa ya kutochukuwa hongo tangu aangie jeshi la polisi.
Posted on: Fri, 09 Aug 2013 23:40:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015