#WAKULIMA WALALAMIKIA BEI YA CHINI YA MAHINDI Wakulima maarufu - TopicsExpress



          

#WAKULIMA WALALAMIKIA BEI YA CHINI YA MAHINDI Wakulima maarufu katika kaunti za Uasin Gishu na Trans~Nzoia wamejitokeza ili kulalalamikia bei ya chini ya mahindi.Wakizungumza katika kikao na washikadau katika sekta ya ukulima kwenye mkutano uliofanyika siku ya Ijumaa, wakulima hao wamedai kuwa Ghala la Kitaifa(NCPB) linawanyanyaza kwa kununua bidhaa iyo kwa bei ya chini mno.Wamekashifu shirika hilo kwa kutepetea kuwahudumia wakulima hao vilivyo kwani wamedai kuwa wananunua mbolea kwa shilingi 3800 wakati wa upanzi na kuuza gunia moja la mahindi kwa shilingi 2000 baada ya kuvuna.Juhudi za kuzungumza na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo hazikufua dafu lakini wakulima hao wameomba serikali kuu kuwashughulikia vilivyo.
Posted on: Sun, 04 Aug 2013 03:39:37 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015