WANNE WAFA KATIKA AJALI 2 TOFAUTI KILOMBERO: AJALI - TopicsExpress



          

WANNE WAFA KATIKA AJALI 2 TOFAUTI KILOMBERO: AJALI JUNI 24, 2013 Watu wa nne(4) wamefariki Dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea Juni 20 na 23 Wilayani Kilombero. Katika ajali ya Kwanza iliyotokea katika eneo la Mikumi Kijiji cha Michenga ,Watu watatu Waendesha Baiskeli wamefariki kwa kugongwa na gari lenye namba za usajili T325 ENP aina ya ISUZU FORWARD lililokuwa likitokea Mlimba kuelekea Ifakara . Watu hao ambao majina yao hayajafahamika wamegongwa majira ya saa moja usiku wa jana na kufariki papo hapo, wanakadiliwa kuwa na Umri kati ya miaka 38 hadi 40. Jeshi la Polisi limesema kuwa Dereva wa Gari hilo ambaye hajafahamika alikimbia huku majina ya Marehemu hayo yakiwa bado hayajafahamika na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea. Katika tukio lingine Mkazi wa Mlabani Athumani Mnyika mwenye umri wa miaka 23 amefariki dunia baada ya mtumbwi alikuwa anasafiria kuvuka Mto Lwipa kupinduka akiwa na familia yake katika eneo la kijiji cha Mofu. Hata hivyo Mke na watoto wameokolewa na Nahodha wa mtumbwi huo huku maiti ya marehemu huyo imeonekana jana na kuzikwa.
Posted on: Mon, 24 Jun 2013 14:30:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015