WARAKA WA MWALIMU…………………………….. NIMEMUOTA - TopicsExpress



          

WARAKA WA MWALIMU…………………………….. NIMEMUOTA MWL.J.K ANANITUMA Amesema Waambie Wanasiasa Wa Nchi Hii Kuwa Tanzania Ni Kubwa Kuliko Wao, Amani Umoja Na Mshikamano Uliopo Haukushushwa Kama Boksi La Zawadi, Ila Ulijengwa Kwa Misingi Kwa Hiyo Waache Kujifanya Wao Ni Miungu Watu. Na wasivuruge misingi hiyo kwa sababu ya hila, uchoyo na taama ya kuuingia ikulu na kwa maslahi ya vyama vyao. Pia Amesema Niwaambie Wanasiasa Wa Nchi Hii Waache Kuwadanganya Wananchi Eti Kila Wanachowaza Au Wanachosema Wao Ni Watanzania Wanasema Au Kuwaza Hivyo. Amesema niwakumbushe kuwa watanzania ni watu wenye upeo,mawazo, fikra, maoni na mitizamo yao kwa hiyo sio muhimu sana kuawasemea watu wenye vichwa wala sio maboksi. Amesema niwaambie watanzania wote kuwa ili tujikwamue kiuchumi ni lazima tujifunze kuchambua budget kama tunavyochambua siasa. Pia amesema budbet hii bado ni zile zile za kuchukuwa toka kwa wasio nacho na kuwaongezea walichonacho kwa hiyo pengo kati walio nacho na wasio nacho bado litaendelea kuwepo, Aidha amesema budget hii 2013/14 bado mrejesho wake kwa masikini ni mdogo ukilinganisha na mchango wao kwa taifa hili na rasilimali tulizonazo. Amesema pia wasomi wameiharibu nchi hii (Tanzania) hasa kwa sababu kila msomi leo anataka kugombea ubunge, kufanya kazi halmashauri na pia kwa sababu wasomi wamegeuka kuwa watu wa lawama badala ya kuwa washauri wa serikali, vyama vya siasa,taasisi za kiraia na makundi mengine. amesema kwa sababu nchi hii imepoteza mwelekeo maana wasomi na wasiokuwa wasomi wote wamekuwa hawana tofauti wote ni watu wa lawama na kukosoa tu, eti wamekuwa wanaharakati. Pia amesema, waliokuwa waalimu wasikimbie hiyo taaluma maana ni taaluma yenye ‘bright future’. ameongeza kuwa hawatastaafu kabla ya mambo yao kuwa mazuri maana taifa makini linawekeza katika elimu kabla ya taaluma au maeneo mengine.Ameongeza kuwa madaraja yatapanda tu na angalau nao wataweza kuongeza pea za viatu na suruali, ila kaomba walimu vijana wapunguze kuvaa vimodo na vimini eti kwa sababu siku hizi watoto wanawahi kubalehe. Amesema katika dhambi kubwa katika karne ya 21,hii ya utandawazi na utandawizi ni kujaribu kuvunja muungano,kwa sababu mataifa makubwa ya kibepari kama ulaya yanafikiria kila kukicha juu ya kuungana zaidi, ni aibu kwa mtanzania, mtanganyika,mnzanzibara au mnzanzibara kuufikiria kuvunja muungano, amesema hii si tu ni hatua sita nyuma katika maendeleo bali pia ni dhambi sawa na kula nyama ya mtu na hatutaishia hapo, tutaendelea katika sera za majimbo na kikanda..n.k Ukweli kanambia mambo mengi nakumbuka nilimkatisha baada ya kuamka niliposikia adhana nilipoamka kwenda kusali alfajiri…lakini inshalah naamini ataendelea tena leo usiku nikilala. naishia hapa sehemu ya kwanza. Nakala kwa; Walimu wote, Wanasiasa wote, Wanaojiita wasomi, Wanaojiita wanaharakati, Wanasiasa wote, Watanzania woooooote popote.
Posted on: Wed, 19 Jun 2013 17:04:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015