WHAT IS BEHIND KAGAME?? Gazeti la Mtanzania la Agosti 22 - TopicsExpress



          

WHAT IS BEHIND KAGAME?? Gazeti la Mtanzania la Agosti 22 limeripoti juu ya hujuma za Rwanda kwa Tanzania. Habari hiyo ilikuwa ndio habari ya kwanza iliyopewa kipaumbele (Lead Story) na ilikuwa na kichwa "RWANDA SASA WAANZA KUIHUJUMU TANZANIA” • Yatangaza kutotumia Bandari ya Dar es Salaam, • Yataka bunge la EAC kukutana Kigali badala ya Arusha. Niliposoma habari hii nilipata taswira mpya dhidi ya Kagame tofauti na nilivyokuwa nikimfahamu awali. Siku moja rafiki yangu alipata kuniambia kuwa Rwanda kujiunga na EAC haikuwa bahati mbaya. Ni mkakati maalum uliosukwa na kuundwa kitaalamu na Kagame akiungwa mkono na Mzee Museveni. Burundi iliingizwa tu ili kufunika kombe maana isingewezekana Rwanda kuwa mwanachama wa EAC na Burundi kuachwa. Inadaiwa mkakati huo maalumu wa Kagame ulikuwa ni kutawala eneo lote la Afrika Mashariki kwa kuhakikisha raia wake wanapenya na kushika nyadhifa mbalimbali katika kila nchi mwanachama. Wapo waliopuuza na kuona si madai ya msingi, lakini hivi majuzi tumesikia aliyekuwa mkuu wa mawasiliano pale usalama wa Taifa kumbe hakuwa Mtanzania, hivyo amerudi kwao Rwanda. Can u imagine? Kuna ukweli kuwa WanyaRwanda walikuwa na mkakati maalumu. Kwa kipoindi ambacho nimekuwa Jumuiya ya Wanafunzi Afrika Mashariki nimeona vitu tofauti sana kati ya wanafunzi kutoka Rwanda na mataifa mengine wanachama wa EAC. Kwanza kwenye vikao vyote vilivyofanyika delegation ya wanafunzi wa Rwanda inakuwa kubwa kuliko nchi nyingine yoyote. Tulipofanya kikao Arusha WaTanzania tulikuwa 46 na WanyaRwanda 67. Walikuwa wengi kuliko hata wenyeji. Nikadhani labda ni kwa sababu Watanzania wana hulka ya kupuuzia so labda kikifanyika nchi nyingine wenyeji watakuwa wengi. Lakini kilipofanyika pale Egaton University sikumbuki idadi ya Wakenya ilikuwa ni ngapi lakini WanyaRwanda walikuwa almost mara mbili ya Wakenya ambao ni wenyeji. Kama hiyo haitoshi kuna suala jingine nililiona kwa hawa ndugu zetu wa Rwanda. Kwa kutumia refference ya kikao cha Arusha, niligundua wanafunzi wa nchi zote walikuja kwa mfumo mmoja isipokuwa wa Rwanda. Wanafunzi kutoka Kenya, Uganda, Burundi na hata wenyeji Tanzania walikuja kwa kugharimiwa na vyuo vyao, lakini wanyaRwanda waligharimiwa na Rais Kagame. Walikuja Arusha na ndege ya sekikali ya Rwanda. Wakisindikizwa na Ulinzi wa Askari wa Rwanda, na Waaandishii wa Habari wa Rwanda ambao walikuwa wakirekodi matukio yote tangu kwenye chumba cha mkutano hadi hotelini kwenye vyumba vya kulala. Kutokana na wingi wao, walishinda nafasi nyingi sana kwenye East Africa Community Students Union. Yawezekena kwa wakati ule tuliona kawaida, lakini kwa sasa tunahitaji tafakuri kuntu juu ya hili. WHAT IS BEHIND KAGAME??
Posted on: Mon, 26 Aug 2013 16:45:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015