Waamuzi 6:30-34 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao - TopicsExpress



          

Waamuzi 6:30-34 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao afe kwa sababu ameibomoa Madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo, Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi;kama yeye ni Mungu na ajitetee nafsi yake kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake.Basi akamwita Yerubaali siku hiyo akisema Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake kwa ameibomoa madhabahu yake.”Unapovunjwa madhabahu ya Baali wenye kumiliki hiyo madhabahu huamka na kuanzisha kisasi juu yako,Bali pale ambampo madhabahu ya Mungu inapovunjwa na mtu Mungu huamka na kufanya kisasi na huyu aliyevunja” Kuna tofauti kubwa sana kati ya hizi madhabahu mbili ya Baali na Mungu kwani kila moja inafanya kazi sawa lakini tofauti kubwa ni manufaa yake na jinsi zinavyojitetea na wakati wa faida zake. Madhabahu ya baali watu huamka juu yake na kuanza kuitetea kwa kukupatia adhabu ikiwemo kuuwawa lakini ile nyingine ni tofauti. Madhabahu ya Mungu inatoa msamaha wa dhambi kwa kifo cha mwanae pale msalabani utapata nafasi ya kujongea kwake na kusamehewa ila ukikataa bado utapata nafasi ya kifikiri kwa maana neno lasema watendao maovu bado wataishi miaka mingi katika shida zao tu hivyo hukumu ya kifo haipo ila kuna hukumu ya Roho wakati wa mwisho kwa maana kimwili utaishi ajapokuwa ulikwisha kufa. Ukiwa na madhabahu ya baali itakupatia kila kitu unachohitaji katika maisha yako mfano-Pesa,Nyumba,Mali nk lakini kuna wakati utadaiwa vitu ambavyo vitakugharimu sana ikiwapo kutoa uhai wa baadhi ya vitu kwa kuanzia huwa wanadai vitu vidogo vidogo tu ambavyo utaona ni kawaida kama vile. (1)Pesa,Chakula,Nywele,baadhi ya viungo vya wanyama nk. (2)Vifaa kama kuchanjwa na kuchinja wanyama – hapo inaanza kukua. (3)Maisha ya baadhi ya jamaa zako wa mbali (4)Maisha ya familia zako kama mke na watoto (5)Maisha yako mwenyewe. Ukiona imefikia kiwango hicho hapo ndio mwanzo wa kwenda na kuishi kuzimu moja kwa moja. Hapo unakuwa umefikia kiwango cha juu maana umepanda vyeo hadi utafikia kuwa mkuu. Hivyo ni bora ukajua ni madhabahu ya aina ipi unayoitumikia na ukaanza kujitoa kwani ni hatari ukiwa upande wa Baali kwa maisha yako wako watu wengi sana utasikia mgaga Yule kataka mbuzi tu kwani kuna shida gani name kesho nitapata pesa sawa umetoa mbuzi je umewahi kujiuliza baada ya mbuzi nini atadai. Madhabahu ya Mungu nayo inataratibu zake nazo ni kama ifutavyo. Mimi ni Mungu wa Maagano hivyo kanuni yake ya kwanza ni kama ifutavyo – (1)Unaweka agano naye La kukiri (2)Agano la Damu ya Yesu – Msalaba. (3)Agano la Kutokuabudu Mungu Mwingine. (4)Agono la kuifuata Sheria au kanuni zake. (5)Kumwabu yeye (kuwa tegemeo lake yeye tu kwa kila jambo) Unapotekekeleza hayo hapo yeye hukulinda na kukubariki kwa kila jambo na hapo utakuwa na uhakika wa kufanyika mwana katika kristo Yesu nawe utarithi ahadi ile ya milele nawe utafanikiwa katika maisha yako yote. Ameni
Posted on: Tue, 30 Jul 2013 06:53:31 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015