Wakati flani huwa namshangaa sana kaka yangu huyu Jusa - TopicsExpress



          

Wakati flani huwa namshangaa sana kaka yangu huyu Jusa (Mwakilishi) kule Zanzibar anapo simimia kwa nguvu nyingi tunataka mamlka kamiri na ikiwezekana tubaki ujirani mwema Hivi huwa anatoa mifano katika mazunguzo hayo? Na je amewaandaa ki saikolojia wazanzibari wanao kaa huku Tanganyaika(Tanzania bara) Mimi nadhani angekuwa amewaandaa vya kutosha Wazanzibari wanao kaa huku Tanzania bara kisaikolojia na wamamuelewa wangekuwa waisha muunga mkono kwa kuanza safari ya kurudi Zanzibari Lakini maajabu kila kukicha wazanzibari wanazidi kununua mitaa na kujenga majumba makubwa means hii nchi ni yetu sote na Tanzani bara ni kwao Kaka Jusa tafakari kwanza hilo tena kwa uzuri zaidi Wapemba wengi wamejenga na kuna mitaa kabisa mpka mtwara mpka Kagera ndani Sasa kaka Jusa unafikilia ni nchi gani ya ujirani mwema itakayo ruhusu baada ya kugawanyika watu wasio wazawa waendelee kumiliki aridhi na majumba? Tunao wakenye tunao Warwanda burundi na kwingine lakin bado katiba inasema aridhi ni mali ya serikali inayo milikiwa na watanzania hawa woote wengine ni wawekezaji na mda ukifika watasepa kwao,sasa unataka na wazanzibari wanao kaa huku waanze kukaa kwa masharti hapana hawa ni ndugu zetu zaidi ya miaka 50 sasa ,tufikilie kuanzia pale tujenge zaidi mifano iko wazi Sudani na sudani ya kusini walipo tengana walifungasha mizigo kwao,korea na korea ya kaskzn na kwingine kaka Jusa na mahili na anayajua sana haya sasa kama anaweza aanze na kuwa comvice Wazanzibar warudi Zanzibar kwanza ili wadai Zanzibar wakiwa wote sio vipande vipande na kama ataweza Alipo yazungmza haya Prof Shivji na alikuwa ameona mbali na juu ya rasimu 2 Serikali 3 ni mzigo kwa serikali zote sio tu kwa Tanganyika lakini pia hata huko kwa wenzetu wazanzibar Leo tuna budgte ya 18 trillion hivi tukianza kuzigawa hizi kwa serikali zote hizo tutabakiwa na nini kwa maendeleo naona budgte kubwa itakuwa katika kuwalipa viongozi na viongozi wastaafu,kuwahudumia magari na familia zao na pesa ya maendeleo hakuna Lakini maana ya kuwa na serikali 3 ni kusema sasa tunakuwa na serikali mbili ambazo zina kuwa na sura sawa katika kila kitu na serikali zote zichangie kuendesha serikali ya muungano ,Nawaulizeni tena marafiki zangu wa Kizanzibar nchi yenyewa ilivyo hivyo kuna kipi ambacho mmejiandaa kukizalisha kiwatosheleze na mbakize cha kuachangia katika serikai ya muungano? Jibu ni hakuna sasa inabidi itakayo kuwa serikali ya Tanganyika ijibebe na ibebe ya Jamhuru ya muungano wa Tanzania na kwa nini Watanganyika wabebe mzigo huo? Yangekuwa ni maamzi yangu ningesema sasa twende katika kuwa na serikali moja tuu na atakaye kataa hapo tumpige viboko Kuna faida nyingi sana kwa Wazanzibar kuliko hata hao Watanganyika 1, Tanganyika ina watu wengi 40 M so ki uchumi na bisahara ni faidia kwa Wanzanibari ambao wao ni wachache 2 Money securation( Mzungko wa pesa) Tanganyika ina watu wengi katika mzunguko wa pesa ni mkubwa ukilinganisha na watu wachache 3, Tanganyika ina aridhi kubwa hivyo ni rahisi kwa ndugu zetu kuja huku na kulima na shughuli nyingin za kibinadmu 4 Ulinzi na usalama tuko wengi na tukiwa wamoja ,umoja ni nguvu 5 Wigo wa ajira ni mkubwa tukiwa wengi hivi kuliko mkiwa wachache humo 6,Tumekuwa marafiki na ndugu kwa mda mrefu Jusa asitutenganishe tu kwa faida moja tu ya kisiasa bado kuna faida nyingi zaidi ya uhuru wa kisaiasa * Ni kweli muungano wetu una matatizo mengi ila mengi ni matatizo ya kisiasa na kisaikolojia tuna weza kuanzaia hapa na kusema basi tuwe na serikali moja tu haya mengine tukamwachia Jussa ** Nawakaribisheni katika mjadala huru Wazanzibari na Watanganyika(Tanzania bara) bila ya matusi**
Posted on: Fri, 06 Sep 2013 19:05:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015