Wananchi wote wa jiji la Dar es salaam mnaopenda Katiba bora yenye - TopicsExpress



          

Wananchi wote wa jiji la Dar es salaam mnaopenda Katiba bora yenye kujali zaidi maslahi yetu sote, vizazi vyetu vijavyo na nchi yetu kwa ujumla siku ya Tarehe 21/09/2013 saa 5 asubuhi tunaombwa kujitokeza kwa wingi katika Maandamano yatakayoanzia eneo la TAZARA kuelekea katika viwanja vya JANGWANI utakapofanyika mkutano Mkubwa wa hadhara kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kutotia saini mswada mbovu uliopitishwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi Bungeni, nia ikiwa ili kupinga na kusitishwa kwa mpango batili wa CCM wanaotaka kupitishwa kwa Katiba mbovu yenye kujali tu maslahi yao na chama chao kuliko maslahi ya Wananchi. Hii ni nafasi pekee kwetu wananchi kutumia haki yetu kikatiba kupata kilicho bora. Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani: CHADEMA, CUF na NCCR wataongoza Maandamano hayo na kuyahitimisha kwa Mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya jangwani. Tunahitaji mabadiliko ya kweli sio katika maneno ya viongozi Feki Tunahitaji Viongozi wanaojua maisha halisi ya Mtanzania
Posted on: Wed, 18 Sep 2013 21:44:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015