Wataalamu wa Umojawa Mataifa waondoka Damascus. Wataalamu wa - TopicsExpress



          

Wataalamu wa Umojawa Mataifa waondoka Damascus. Wataalamu wa maswala ya kemikali wa Umoja wa Mataifa UN waliokuwa nchini Syria wameondoka asubuhi ya leo jumamosi baada ya kukamilisha uchunguzi wao wa kubaini iwapo silaha za kemikali zilitumikakatika mapigano. Wataalamu hao wamekamilisha uchunguzi wao wa siku nne katika eneo linalolalamikiwa kuwa silaha za kemikali zilitumika dhidi ya raia pembezoni mwa mji mkuu Damascus tarehe 21 ya mwezi huu. Jumla ya Wachunguzi hao 13 wanaoongozwa na Ake Sellstrom wameondoka kupitia Beirut nchini Lebanon ambapo walionekana wamebeba mizigo yao katika magari saba ya UN. Kuondoka kwa wataalamu hao kunatajwa kama hatua mojawapo ya kukaribia kupata ukweli unaotafutwa sambambana kujua mustakabali wauamuzi wa uvamizi wa kijeshi unaopigiwa upatu na Marekani. Maafisa wa Umoja wa Mataifa UN wanasema itachukua majuma mawili kupata majibu ya utafiti huo na kukabidhi ripoti kwa Katibu Mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon. Chanzo: RFI
Posted on: Sat, 31 Aug 2013 07:57:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015