Watanzania wenzangu hebu turekebishe haya tuliyoyazoea sana mpaka - TopicsExpress



          

Watanzania wenzangu hebu turekebishe haya tuliyoyazoea sana mpaka kuyahalalisha ingawa ni makosa: 1. Barca, kifupi cha Barcelona kinatamkwa BASA siyo Baka. Tutamke kwa usahihi BASA. 2. Kujihami au kujilinda tukikuchanganya na kiingereza, tunapaswa tukuite KU-DEFEND na siyo ku-defence kwa sababu "to defend" ni kitendo KULINDA lakini "defence" ni jina au nomino ULINZI. Usahihi ni kusema wana-DEFEND na siyo "wana-defence" isiyo na maana yoyote ile. Hebu twende hivyo. 3. Siku hizi kuna wataalam wa soka kadhaa wa Tanzania wanaosema kwamba kuna handball kama mkono ndiyo unaufuata mpira na "ball hand" kama mpira ndiyo unaufuata mkono. Hapana, neno pekee la kutumika katika muktadha huo na HAND BALL. Kwa hiyo ni sahihi ukisema ""handball" hii ni sahihi kwani mkono ndiyo umeufuata mpira lakini "handball" ile haikuwa sahihi kwa sababu mpira ndiyo ulifuata mkono". Ball hand kama ina maana yoyote ya kiingereza, maana hiyo ni ama mkono uliotengenezwa kwa mpira wa kuchezea soka au mkono ulio kama mpira wa kuchezea soka. Jamani hakuna "ball hand" kwenye soka bali HAND BALL tu. 4. Kibao cha namba ya gari ni NUMBER PLATE na si plate number. Number plate maana yake ni kibao cha namba wakati plate number inamaanisha namba ya kibao. Kwa maana ya plate number, kitakachozungumzwa hapo ni kama vibao hivyo vina namba 1,2,3,4,5 na kuendelea kwa mfano "hii ni plate number 3" au vinginevyo kuizungumza namba yenyewe ya kwenye kibao na si kibao chenyewe kama T 467 ASN lakini ni sahihi kusema "number plate ya gari langu imekunjika". Hivi vibao vya namba za magari ni NUMBER PLATES na si plate numbers. Hebu tubadilishe hapo.
Posted on: Wed, 17 Jul 2013 00:01:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015