Watu wengi huwa wanauliza..inakuwaje mtu anaomba kubreak-Up na - TopicsExpress



          

Watu wengi huwa wanauliza..inakuwaje mtu anaomba kubreak-Up na wewe na ukimuuliza sababu anakwambia HANA…Unamforce weeee,niambie baby,,,sema anything I will do jamaniii,don’t leave me..anakusisitizia HANA SABABU ila anataka muachane…Inatokea..Sio kila Uhusiano huwa umejengwa kwenye mawe…Mahusiano mengine yamejengwa kwenye uji wa ulezi,mkitembea kidogo tu mnagundua njia nzima ina utelezi hamtafika..Kuna CRUSH..mtu mnakutana mnazimikiana,mnaenda kidogo tu miezi mi3 zile Spark za Mahaba zimeisha na wala haupretend ndo imetokea,CRUSH IMEKUFA…Usiforce moto wa mshumaa uivishe sufuria la makande…Mwambie tu,mwanangu ule mzuka umekata! Huwa hawaelewagi,especially wanawake,yaani atakuforce umwambie amekosea wapi…au babe niache kuvaa magauni marefu,eti babe au ninyoe nywele…wala hizo sio sababu…ZUKA LIMEKATA Sasa wale Asha Ngedere utawapenda..Wanaambiwa Its over hawaelewi somo,utawasikia HAACHWI MTU HAPA,NTAPIGANIA NAFASI YANGU...Upigane kwani Mapenzi yana Vita vya Majimaji kujifanya Kinjekitile Ngwale….Hisia zinakufa kwa Wanandoa sembuse wewe Girlfriend??Waulize waliooana kama Betri huwa haziishi maji wanaishi kwa Kuboost…Waulize wakwambie. Usimlazimishe mgonjwa wa Kisukari kunywa Fanta Orange,UTAMUUA!
Posted on: Sat, 16 Nov 2013 19:18:46 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015