Wednesday, 03 July 2013 17:15 Njama za Mawahabi za kutaka kuzusha - TopicsExpress



          

Wednesday, 03 July 2013 17:15 Njama za Mawahabi za kutaka kuzusha fitina katika ulimwengu wa Kiislamu font size decrease font size increase font size Print Add new comment Wapiganaji wa Kiwahabi wanaotekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wengine. Wapiganaji wa Kiwahabi wanaotekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wengine. As-Salamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kujumuika nami katika kipindi kingine cha makala ya wiki ambacho leo kitaangazia njama za Marekani za kutaka kuwagawa Waislamu kupitia Masalafi wa Kiwahabi, karibuni. Hivi sasa ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na njama zanazofanywa na maadui wake. Kwa upande mmoja, harakati za mwamko wa Kiislamu zilizozikumba tawala vibaraka kuanzia huko kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati, zimetia dosari maslahi haramu ya madola yanayopenda kujitanua duniani. Kwa upande mwingine harakati hizo zinakabiliwa na njama hatari zenye nia ya kuzusha tofauti na vita kati ya makundi tofauti ya Kiislamu kwa manufaa ya madola hayo yenye kupenda kujitanua ya Magharibi na vibaraka wao katika eneo. Ni kwa ajili hiyo ndipo yakaingizwa katika uwanja huo makundi ya Masalafi wa Kiwahabi yanayokufurisha na kutekeleza vitendo vya kinyama dhidi ya Waislamu. Hivi sasa Syria imegeuka na kuwa uwanja wa kuzushwa tofauti na mifarakano kati ya Waislamu. Baada ya madola ya Magharibi yakishirikiana na waitifaki wao katika eneo kushindwa kufikia malengo yao machafu ya kuiangusha serikali halali ya Damascus, sasa yanafanya njama za kuwasha moto wa vita vya kimadhehebu na kikabila nchini humo kwa kuyasaidia na kuyaunga mkono makundi ya Kisalafi yenye kukufurisha Waislamu na kueneza fikra zinazokwenda kinyume kabisa na mafundisho ya Kiislamu. Kile kinachoshuhudiwa leo katika eneo na kudaiwa kuwa eti ni mivutano baina ya Usuni na Ushia, kwa hakika sio mivutano kati ya madhehebu hayo mawili ya Kiislamu. Hii ni kwa sababu kwa miaka mingi madhehebu hayo yamekuwa yakiishi pamoja kwa amani na kushirikiana katika kila nyanja na kamwe hayakuwahi kuingia katika mapigano na mauaji baina yao. Hatukani kuwa tofauti za kimadhehebu kati ya Usuni na Ushia zimekuwepo, lakini zimekuwa zikidhibitiwa na kutatuliwa kwa amani na njia za kielimu. Ukweli ni kuwa, fikra za Uwahabi na mwenendo wake wa kumkufurisha kila mtu, haziishii tu kwa wafuasi wa madhehebu ya Kishia, bali kikundi hicho pia kinawakufurisha hata baadhi ya wafuasi wa madhehu ya Usuni na wafuasi wa dini nyingine sambamba na kuhalalisha damu zao. Marekani na watawala vibaraka katika eneo walipatwa na wahaka mkubwa, baada ya Imam Khomein (MA) kuongoza ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuhuisha Uislamu halisi ulioletwa na mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAW). Hii ni kwa kuwa kauli mbiu ya dini Tukufu ya Kiislamu inasisitiza juu ya uhuru wa kujitegemea na kupambana na udikteta wa ndani na ukoloni wa nje. Aidha mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, hayakuwa mapinduzi ya Kishia tu. Jambo lingine ni kwamba, mapinduzi hayo yalibeba ujumbe wa uhuru na uadilifu, si kwa ajili ya Waislamu pekee, bali kwa wanadamu wote duniani. Kwa hakika Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yaliibua wangwi wa tetemeko kubwa katika eneo na kuathiriwa harakati za Kiislamu na mapinduzi hayo adhimu. Suala hilo liliwatia hofu kubwa Wamagharibi na kupelekea Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa wakati huo Henry Kissinger kuyazungumzia mapinduzi hayo kwa kusema kuwa, kama utawala mwingine kibaraka katika eneo ungeanguka kwa kukumbwa na mapinduzi kama hayo ya Kiislamu, basi mapinduzi hayo yangepanuka katika nchi nyingine za eneo. ************************************************ Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini hapa, Marekani, madola ya Ulaya na utawala haramu wa Kizayuni, zilifikiria njia ya kukabiliana na wimbi hilo na kutaka kuyabana katika mipaka ya Iran ili yasipate kutoka nje. Isitoshe, madola hayo yenye kupenda kujitanua, yalianzisha mibinyo ya kisiasa, kiuchumi na hata kumchochea dikteta Saddam Hussein wa Iraq kuanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hayo yalifanyika ikiwa ni katika fremu ya kukabiliana na mfumo wa Kiislamu na kupambana kifikra na kiutamaduni na mitazamo sahihi ya kujitegemea iliyokuwa ikilinganiwa na Imam Khomein (MA), Mwasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Kwa ajili hiyo kulianzishwa semina mbalimbali katika vyuo vikuu vya mjini Haifa na Tel Aviv huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa kibaguzi wa Israel, nchini Marekani na katika nchi mbalimbali za Ulaya, sambamba na kuwaalika wataalamu wa masuala ya Mashariki kwa lengo la kuchambua na kung’amua pande za kiitikadi za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Lengo kuu la kufanyika semina na mikutano hiyo lilikuwa ni kuchunguza athari na chanzo cha mapinduzi hayo makubwa. Katika vikao hivyo, watu hao waligundua kuwa, asili ya fikra ya mapinduzi, ilitokana na fikra sahihi za Ushia zenye kufuata mafundisho matukufu yanayotokana na mapambano ya kupinga dhulma ya Imam Hussein, mjukuu wa Mtume (saw) huko Karbala nchini Iraq. Walitambua pia kuwepo kundi linalofahamika kwa jina la Uwahabi ambalo linawakufurisha Mashia. Kwa ibara nyingine ni kuwa natija kamili ya vikao hivyo huko Ulaya na Marekani, ilikuwa hii kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran ambayo msingi wake mkubwa ni kupambana na dhuluma, yana adui anayefahamika kwa jina la Uwahabi na ni lazima kundi hilo litumiwe dhidi ya mapinduzi hayo. Hii ni katika hali ambayo nchini Iran hapakuwahi kusikika suala la Usuni wala Ushia, bali kila mtu akizungumzia mapinduzi ambayo yalileta mabadiliko makubwa katika uwiano wa kieneo. Ghafla utawala wa Iran ulibadilika na kuwa nguvu muhimu yenye kuwaunga mkono watu wanyonge hususan raia madhlumu wa Palestina, suala ambalo lilitakiwa kuzuiwa na Wamagharibi. Kwa ajili hiyo, katika kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Marekani na nchi tofauti waitifaki wake zilianzisha wimbi la propaganda dhidi ya Ushia. Propaganda hizo zilisimama juu ya mambo mawili: Mosi, kuzusha tofauti za kihistoria na kuibua kadhia ya Ufarsi na Uarabu na pili, kuzusha tofauti za kimadhehebu kati ya Masuni na Mashia. Sambamba na kujaribu kuonyesha kuwa Iran na Ushia ulikuwa tishio kubwa kwa ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, maadui hao walisisitiza kupitia vyombo vya habari na siasa zao za eneo kuwa, Wairan ni Mashia na Wafarsi tu ambao hawana mahusiano yoyote na ulimwengu wa Kiarabu wala Usuni. Aidha kwa mujibu wa propaganda hizo zisizo na ukweli wowote, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilidaiwa kuwa na lengo la kuwafanya Masuni kuwa Mashia kwa kutumia jina la dini ya Kiislamu. Hii ni katika hali ambayo Mapinduzi ya Kiislamu, yalikuwa mapinduzi ya kiutamaduni huku ujumbe wake wa kukabiliana na dhuluma, kulingania usawa na umoja, ukitoka katika kitabu cha Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW). Lengo la mapinduzi hayo kwa hakika lilikuwa ni kufikisha ujumbe huo kwa Waislamu na kila mtu mpenda uadilifu duniani. Viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu hawakuwa na lengo la kueneza Ushia, bali kwa mara zote walikuwa na wangali wanasisitiza na kulingania umoja na maelewano baina ya Waislamu. Ni katika fremu hiyo hiyo ndio maana tangu miaka ya kwanza ya Mapinduzi ya Kiislamu, kukawa kunafanyika vikao mbalimbali vinavyohudhuriwa na maulama wa Kisuni na Kishia kutoka pembe zote za dunia hapa mjini Tehran kwa lengo la kuimarisha umoja na mashikamano katika umma wa Kiislamu. Huku hayo yakiendelea, Marekani na waitifaki wake katika eneo, wamekuwa wakifanya njama za kupotosha uhalisia wa mapinduzi hayo na ujumbe wake, sambamba na kuyataja Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ya Kishia na ambayo ni hatari kubwa kwa nchi nyingine hususan zile za Kisuni. ********************************************* Katika kuendeleza siasa za Marekani na waitifaki wake kwa ajili ya kupambana na fikra na itikadi za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kuliasisiwa shule mbalimbali za Kiwahabi huko nchini Pakistan, Afghanistan na hata nchi za Asia ya Kati, ambapo walilelewa makumi ya maelfu ya wanafunzi wa Kiwahabi kwa msingi wa fikra za kuwakufurisha Waislamu za Ibn Taymiya. Katika shule hizo mafundisho pekee yaliyotolewa na yangali yanatolewa ni kuwaua Mashia eti kwa ajili ya kwenda peponi. Asili ya mpango huo, uliratibiwa na mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter Bwana Zbigniew Brzezinski, ambapo sambamba na kufanya safari nchini Pakistan, na kwingineko alisimamia vizuri mpango huo. Kundi la Taleban lenye kufuata misimamo mikali na potofu huko nchini Afghanistan, liliasisiwa chini ya mpango huo huo, ambapo kwa msaada wa kifedha na kiusalama wa Marekani, Uingereza na Pakistan, lilifanikiwa pia kudhibiti asilimia 90 ya ardhi yote ya nchi hiyo sambamba na kuwafurusha nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Kabul wapiganaji wa Mujahidina katika kipindi cha muongo wa 1990. Baada ya ushindi wa muqawama wa Kiislamu huko kusini mwa Lebanon mwezi Agosti mwaka 2006, Marekani na waitifaki wake walieneza fikra zisizosahihi za Masalafi wa Kiwahabi katika baadhi ya nchi za eneo. Aidha ushindi huo mkubwa wa Hizbullah dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni, ulizikosesha usingizi Marekani, utawala bandia wa Israel na tawala za kiimla za falme za Kiarabu katika eneo, ambapo bendera ya manjano ya Harakati hiyo ya Hizbullah na picha za Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wake, zilionekana katika miji mikuu na miji mingine ya nchi nyingi za Kiarabu. Ushindi huo uliongeza uungaji mkono kwa harakati hiyo katika eneo ambapo shakhsia mkubwa wa Kisuni Sheikh Rashid al-Ghannushi wa Tunisia aliongea kwa simu na Sayyid Hassan Nasrullah kwa kusema kama ninavyomnukuu: “Wewe ni kiongozi wangu.” Mwisho wa kunukuu. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa Marekani Bi Condoleezza Rice mwezi Oktoba mwaka 2006 alifanya safari mjini Cairo na kwa mara ya kwanza badala ya kukutana na Waziri mwenza wa Mambo ya Nje wa Misri, alitaka kukutana na viongozi wa usalama wa nchi nne za Kiarabu. Wakuu hao wa vyombo vya upelelezi na usalama kutoka Misri, Jordan, Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu walikutana na waziri huyo wa mambo ya nje, ajenda kuu ya mazungumzo yao ikiwa ni kupanua zaidi Uwahabi, kuzusha tofauti za kimadhehebu baina ya Suni na Shia na kuchafua jina la Harakati ya Hizbullah. Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa utawala bandia wa Kizayuni Tzipi Livni alinukuliwa akisema kama ninavyo mnukuu: “Njia pekee tuliyonayo ni kuzusha tofauti kati ya Shia na Suni katika eneo hili.” Mwisho wa kunukuu. Kama hiyo haitoshi viongozi wa utawala wa Kizayuni hususan Meir Dagan mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israel MOSSAD alitangaza kwa mara kadhaa kuwa, njia pekee ambayo ingesaidia kulinda usalama wa utawala huo bandia, ni kuzusha tofauti za Usuni na Ushia baina ya Waislamu na kuzusha mapigano ya kimadhehebu katika ulimwengu wa Kiarabu. ************************************************ Mgogoro wa Syria na njama za kuangusha serikali ya nchi hiyo, kwa hakika ni mwendelezo wa njama hizo hizo za kuzusha tofauti kati ya Usuni na Ushia. Kwa mtazamo wa Mawahabi, ni halali kumwaga damu ya kila Suni anayepinga fikra za Kisalafi na za kuwakufurisha Waislamu. Ukweli ni kuwa yote hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa mashirika ya kijasusi ya Marekani na waitifaki wake katika eneo. Watu wanaolipua misikiti ya Kishia nchini Iraq na Syria, ndio wale wale wanaolipua misikiti ya Kisuni katika nchi tofauti. Hii ni kwa kuwa Msuni wa kweli hawezi kutekeleza vitendo kama hivyo vinavyokwenda kinyume na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. Wapenzi wasikilizaji, kipindi chetu cha makala ya wiki kinaishia hapa kwa leo. Ni matumaini yangu kuwa mmenufaika vya kutosha na kuweza kufahamu njama za Marekani na waitifake wake, za kutaka kugonganisha na kuwagawa Waislamu kupitia Mawahabi. Mwandaaji na msimulizi wa makala hii ni mimi Sudi Jafar Shaban nakuageni kwa kusema: kwaherini. HIKI NICHOMBO CHA KHABARI KINACHO IHUDUMIA IRANI, LAKINI, NINGESHAURI IKIWA KUNA WATU WAKARIBU WANAO UHUSIANO NA CHOMBOHIKI HUKO IRNI, WAWASHAURI, NA KUWAKUMBUSHA YAKUA WAO NDIO WANZISHI WA FITNA WAKWANZA. KWAUSHAHIDI NIKUA KWANZA WANAONGEA WASICHOKIJUA. NIMESTAAJABISHWA SANA SEHEMU MOJA , WANASEMA MAWAHABI WANAZUA FITNA, KISHA SEHEMUNYINGINE WANAHALALISHA DAMU YA KILA SUNNY ANAE KWENDA KINYUME NA FIKRA ZA KISALAFIY, EEEEDA? NINI WANASEMA HAWAVIBARAKA WA KISABAI? HAWAJUI HATA WANACHOKIONGEA, KISHA IKIWA HAO WANAZUA FITNA INAKUAJE UNATANGAZA IKIWA HUTAKI FITNA? BIMAANA UNATANGAZA ILIKUZIDISHA CHUKI UPANDE MWENGINE WATU WAWACHUKIE HAWA, NA OOTE WANAO NASIBISHWA KATIKA DHEHEBUHILO.SIJAONA MAJUHA KAMA HAWA.
Posted on: Fri, 19 Jul 2013 01:36:22 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015