Wito Kwa Mashia Wenye Akili Itikadi Potofu Mamduwh - TopicsExpress



          

Wito Kwa Mashia Wenye Akili Itikadi Potofu Mamduwh Al-Harbiy Imefanyiwa Kazi Kiswahili Na: Muhammad Faraj As-Saay Na Muhammad Baawazir Napenda kuzungumza katika mlango huu kuhusu maudhui haya ninayopenda kuyaita, “Wito Kwa Mashia Wenye Akili”. Na mazungumzo yangu ni ibara ya utata mwingi nilioupata katika madhehebu haya ya kishia, na nimependa kuwahutubia nao hao wenye akili, hao ambao wanatafiti haki miongoni mwa vizazi vya Mashia pengine watapata jawabu katika utata huu ambao nimeuona umejaa katika vitabu vya Kishia. Na huo ni utata unaobainisha mgongano katika itikadi hii, na huenda nikaifafanua kwa haraka haraka kwani ni mengi ya kuandikwa, na nataka kutoka kwa hao wenye akili wanaofanya utafiti wa haki wajivue na wafanye ikhilasi kwa nia zao kwa ajili ya Allaah Ta’alaa na wachambue utata huu ikiwa ni kweli wako hivyo. Na mimi sishuku kuwa wao wanatafuta ukweli. Miongoni Mwa Utata Unaopingana Kwa Mashia. Kwanza: Mashia wanaamini kuwa ‘Aliy ni Imamu aliyehifadhiwa ‘Ma’aswuum[1], kisha tunamwona kwa kukiri kwao wenyewe kuwa amemuozesha mwanawe wa kuzaa Umu Kulthuum, dada wa Hasan na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamuozesha ‘Umar bin Khatwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) Na hili limethibitika kwenye vitabu vyao vyenye kutegemewa kwa Mashia, yaani: Kuthibitika kwa ndoa hii imeandikwa katika kitabu cha Kulayn kinachoitwa, ‘Al-Kaafi’ katika Juzuu ya Sita Uk. 115 na vile vile katika kitabu: “Tahdhiibul-Ahkaam” cha Tuus, na kitabu, “Al-Istibsaar”. Vile vile na vitabu vingi vyenye kutegemewa kwa hiyo ikiwa ‘Aliy bin Abi Twaalib na yeye ni Imamu Ma’aswuum aliye hifadhiwa anamuozesha binti yake Umu Kulthuum dada yake Hasan na Husayn kwa ‘Umar bin Khatab. Kwa hiyo Mashia itawalazimu moja ya mambo mawili kila utamu wa mawili hayo ni uchungu. Ya Mwanzo: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) sio Ma’aswuum, kwa kuwa amemuozesha mwanawe kwa kafiri, na hii inatengua misingi ya madhehebu ya Shia bali inaonyesha kuwa wengine miongoni mwa Maimamu sio Ma’aswuum. Ya Pili: Inalazimika kuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab ni Muislamu ambaye ‘Aliy ameridhia kumuozesha mwanae na kuwa mkwewe, na hili linapinga itikadi ya Shia, kwa kumkosoa kwake na kumkufurisha ‘Umar, na jawabu hizi mbili ndio msingi wa utata huu. Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) walikuwa makafiri, kisha tunaona kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye ni Imamu Ma’aswuum ameridhia ukhalifa wao, kwa hiyo hili linalazimisha kuwa sio Ma’aswuum kwa sababu aliwabai’ (aliwapa mkono wa utii) makafiri na wala hakuwaasi, na alikiri ukhalifa wao, na jambo hili yaani! Kukubali kuwabai hawa makafiri wawili madhalimu – Allaah Atulinde – kuna vunja huko kuhifadhiwa – na ndani yake ni kusaidia udhalimu (dhulma). Na hili halitokei kwa Ma’aswuum abadani. Ama jambo jingine: Ni kuwa kitendo cha ‘Aliy ni kitendo cha sawa wakati alipowabai’ Abu Bakr na ‘Umar kwa kuwa makhalifa hawa wawili walikuwa waumini, wa kweli waadilifu kwa hiyo Mashia katika hilo wanakuwa wamemkhalifu Imamu wao kwa kuwakufurisha na kuwatukana na kuwalani na kukosa kuuridhia ukhalifa wao. Na sisi wakati tunapojiuliza tunaangukia katika mshangao katika mambo yetu, ima tufate njia ya Abul Hasan na Husayn katika kuwasifu Makhalifa wawili, au tufuate njia ya Mashia wafuasi wake waasi ambao wanamtukana Abu Bakr na ‘Umar katika mema yao, na huu ni mushkeli tunaotaka ujibiwe! Utata Mwengine: ‘Aliy alioa wanawake wengi baada ya kifo cha Faatwimah, na hapa tunataka tusikilize vizuri utata huu, na tunataka jawabu la wazi toka kwa wanazuoni wa Kishia. Ninasema: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alioa wanawake wengi baada ya Faatwimah na wanawake wote hao wamemzalia watoto mfano wao ni ‘Abbaas bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, ‘Abdullaahi Bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, Jaafar bin ‘Aliy bin Abi Twaalib, ‘Uthmaan bin Ali bin Abi Twaalib, hao wote mama yao ni mjakazi Binti Hizaam ni Daarim. Na hili limetajwa katika kitabu, ‘Kashful-Ghummah Fil Ma’arifatil – Aimmah’ cha ‘Aliy Al-Arbaly na huyo ni katika Maimamu wa wanazuoni wa Kishia, na pia yuko pia katika watoto wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ‘Ubaydullah bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na Abu Bakr bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na huyu nae mama yao ni Laylaa bint Masuud Daaramiyah, hili pia amelitaja Al-Arbaly katika ‘Kashful-Ghummah’ Na pia yupo Yahya yaani: Miongoni mwa watoto wa ‘Aliy bin Abi Twaalib na Muhammad Al-Asghar na ‘Aun bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Asmaa binti Umaysi. Pia yuko Ruqayyah binti Ali bin Abi Twaalib, yupo pia ‘Umar bin ‘Aliy bin Abi Twaalib na ‘Umar huyu alikufa akiwa na miaka thelathini na tano na huyu ni tumbo moja na Ruqayyah binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Ummu Hubayb binti Rabi’ah hilo pia amelitaja mwenye kitabu ‘Kashful Ghumah’. Pia yupo Ummu Hassan binti ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Ramlah Al-Kubraa binti ‘Aliy bin Abi Twaalib na mama yao ni Ummu Masuud binti Urwah bin Masuud Thaqafi. Swali na utata ambao tunataka ujibiwe na wenye wanazuoni wa Kishia ni, Je, inawezekana kwa mtu kuwaita wanawe kwa majina ya adui zake wakubwa? Awaite ‘Umar, ‘Uthmaan, na Abu Bakr? Hivi mtu mwenye akili atawaita wapendwa wake kwa majina ya adui zake? Je mnajua kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib ndie Mkureishi wa kwanza kuwaita wanawe kwa majina ya Abu Bakr na ‘Umar? Yeye ni Imamu ‘Aliy bin Abi Twaalib, kwa hiyo tunataka tutatuliwe mushkeli huu, na tunataka majibu sahihi ya wazi ili wana akili wa Shia wajue haki. Utata Mwengine: Ndani ya kitabu cha ‘Nahjul-Balaaghah’ ukurasa wa 136, Na hicho ni kitabu cha kutegemewa kwa Mashia, imeandikwa kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikataa ukhalifa, akasema: “Niacheni na tafueni Mwengine”, Imamu Ma’aswuum wa kwanza kwa Mashia anasema niacheni tafuteni Mwengine. Nasema: Hii inaonyesha ubatilifu wa madhehebu ya Shia, kwa kuwa vipi anakataa ukhalifa na huu ukhalifa ni faradhi kutoka kwa Allaah tena ya lazima kama vitabu vya Shia vinavyodai, na vipi ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaikataa nguzo ya kwanza kwa Mashia, nayo ni nguzo ya Uimamu? Anasema: ‘Niacheni tafuteni Mwengine?’ Utata Mwengine: Mashia wanadai kuwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) ambaye ni Mtoto wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye Bibi mtukufu. Mashia wanadai kuwa Bi-Faatwimah amedhalilishwa wakati wa uongozi wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kiasi cha kuvunja mbavu yake wakati watu wakiunguza nyumba yake na kusababisha kutoka kwa mtoto wake kabla hajazaliwa ambae alikuwa alikusudiwa aitwe kwa jina la Al-Muhsin au Muhsin, swali tata ni kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib alikuwa wapi Bi-Faatwimah akifanyiwa haya yote? Alikuwa wapi Simba wa Masimba? Alikuwa wapi shujaa yule? Kwa nini hakuchukua haki ya mke wake Bi-Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) binti wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Hili ni tatizo na swali muhimu lapasa kujibiwa. Utata Mwengine. Tumepata mengi kutoka kwa wakuu wa Kiswahaba wanaingiliana kwa kuoza na kuoa na si hivyo tu bali hata kinyume chake wameoana na Ahlul-Bayt (‘Alayhimus Salaam) Hususan Abu Bakr na ‘Umar, na hili limeafikiwa na wana historia na baina ya wenye kuhamisha habari kutoka kwa Sunni na kutoka kwa Shia, kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemuoa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha). Na vile vile amemuoa Hafswah bint ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye akamuozesha mwanawe Ruqayyah, Kisha Umu Kulthuum kwa Khalifa wa tatu Bwana mkarimu, mwenye staha ‘Uthmaan Bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kwa ajili hiyo alipewa Laqab[2] ya Dhuu Nurayn (mwenye nuru mbili). Kisha mwanawe ‘Uthmaan bin ‘‘Affaan aitwae Abaan alimuoa Ummu Kulthum binti ‘Abdullaah bin Jaafar bin Abi Twaalib. Kadhalika Marwaan Bin Abaan bin ‘‘Uthmaan alimuoa Umul-Qasim bint Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib. Kadhalika Zayd bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Salama binti Al-Husayn na ‘Abdullaah bin Amri bin ‘Uthmaan alimuoa Faatwimah bint Al-Husayn bin ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu). Inatutosha kutaja Makhalifa watatu (Radhiya Allaahu ‘anhum) bila ya kuwataja wengine. Swali linalojitokeza hapa ni kwa nini kukosolewa huku kwa Makhalifa hawa watatu peke yao? Na kwa nini kukoselewa hawa watatu tu na kudaiwa kuwa eti walikufuru na kuritadi”. Hata hivyo wanazuoni wa Kishia hawaweki wazi mbele ya wengine na mbele ya Waislamu isipokuwa wenye akili katika Mashia wanaojua kwa yakini kuwa wanazuoni wao wanamtukana Abu Bakr, ‘Umar, na ‘Uthmaan ndani ya Husayniyaat[3], basi ni kwa nini Maimamu wa Kishia wanawaozesha binti zao kwa watoto wa watu hao? Ama waliowaita watoto wao kwa jina la ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika Maimamu miongoni mwao ‘Aliy kama tulivyotaja punde, alimwita mwanae ‘Umar Akbar na mama yake kama tulivyotaja ni Ummu Habiib binti Rabiiah, ‘Umar huyu aliuawa maeneo ya Karbalaa Tuff yaani katika usiku pamoja na ndugu yake Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) wala haitajwi kabisa kuwa ‘Umar alikufa kwa kuuawa –akiwa Shahidi – kwa Allaah, wala hatajwi katika maombolezo ya Husayniyaat wakati wa msiba wa Husayn na wakati wa kupokea taazia (rambirambi) ambayo inaitwa rambi rambi ya Husayn, hawamtaji ‘Umar. Kadhalika Hasan bin ‘Aliy aliwaita wanawe majina ya Abu Bakr na’Umar na hili lipo katika vitabu vya Shia ‘Al-Irshaad’ cha Mufiid, ukurasa wa 194 na vile vile katika kitabu cha ‘Muntahal-Aamal’ Juzuu ya Kwanza ukurasa wa 240. Vile vile katika kitabu ‘Jalaaul-‘Uyuun’ cha Majlisy ukurasa wa 582. Kwa nini hawatajwi hao? Basi kwa nini wanawatukana hao (Radhiya Allaahu ‘anhum) utata ni mwngi tutautaja hapa kwa haraka haraka. Utata Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’ sikilizeni vizuri, nasema: Kulayn ametaja katika kitabu chake, ‘Al-Kaafii’ kuwa Maimamu wanajua lini watakufa na kuwa wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao, na hili limeandikwa katika ‘Usuulul- Kaafi’ cha Kulayn Juzuu ya Kwanza, ukurasa wa 258 Kulayn aliweka mlango kwa kauli yake, ‘Hakika Maimamu wanajua lini watakufa, na wao hawafi isipokuwa kwa hiari yao’. Kisha akataja Majlisy katika kitabu chake ‘Bihaaru Al-Anwaar’ Juzuu ya 3, ukurasa wa 364, Anasema: “Hakika Maimamu wanajua lini watakufa. Na kuwa wao watakufa kwa hiari yao” na hili lipo katika, ‘Al-Kaafi’, Al-Majlis katika kitabu chake anataja hadithi inayosema: “Hakuna Imamu yoyote isipokuwa amekufa kwa kuuwawa au kwa sumu.” Na hapa kuna utata Mwengine tunasema: Ikiwa Imamu anajua ghaibu, kama alivyotaja Kulayn. Na vile vile ametaja Al-Hurul Al-’Amily, ‘Kuwa iwapo Imamu huyu Ma’aswuum anajua ghaibu, kwa hiyo atajua kinacholetwa kwake, katika vyakula na vinywaji, na akijua kuwa chakula au maji kina sumu atajiepusha nacho. Na hapana budi ajiepushe nacho, na akila chakula hicho atakufa hali ya kuwa amejiua kwa kuwa yeye kwa itikadi ya Shia, anajua kuwa chakula hiki kina sumu akila atakuwa amejiua’. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa, “Mwenye kujiua mwenyewe ni mtu wa motoni”, Je Shia wanaridhia hili. Kuhusu Maimamu, nyinyi mnasema kuwa: “Maimamu wanajua ghaibu, na wanajua lini watakufa.” Majlisy anasema: “Hawi Imamu isipokuwa amekufa kwa kuuwawa au kwa sumu.” Kwa hiyo akiletewa chakula nae anajua kina sumu akala, huku kutakuwa ni kumtukana Imamu huyu, kwani atahesabiwa ni punguani, na hali ya kuwa wao wametakaswa na hili. Kwa hiyo tunataka majibu ya mushkeli huu. Utata Mwengine: Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) alijiuzulu kwa Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika wakati ambao wafuasi wakimnusuru walikuwa wakikusanyika kwake na kuunda jeshi na neema kukusanya itakayomuwezesha kuendeleza vita dhidi ya Mu’aawiyah katika hali hii ndugu yake Husayn alitoka kwa ajili ya kupigana na Yazid akiwa na watu wa chache katika familia yake, katika wakati ambao angeweza kujisalimisha. haiwezekani mmoja wao kuwa katika haki na mwengine kuwa katika batili, kwa sababu iwapo Hasan alijiuzulu pamoja na kuwa na nguvu na jeshi lenye kumuwezesha vita, kwa ukweli kutoka Husayn bila nguvu akiwa dhaifu pamoja na kuweza kwake kujisalimisha, hili lilikuwa ni batili na kosa kwake yeye Husayn kwa kuwa kama Husayn kutoka pamoja na udhaifu wake ni haki, basi kujiuzulu Hasan pamoja na nguvu alizokuwa nazo ni batili. Na hili linawaweka Shia katika eneo wasilohusudiwa ndani yake, kwa kuwa wao wamesema: Hao wote Hasan na Husayn walikuwa katika haki, kiukweli ni kwamba wao wamekusanya mambo mawili yenye kupingana na kauli hii inavunja misingi ya Itikadi ya Shia kwani wakisema ubatili wa Hasani italazimika mbali wa Uimamu wake na wakisema ubatilifu wa Uimamu wake italazimu kubatilika Uimamu wa baba yake kwani ndie aliyemteua. Na yeye ndie aliemsimika baada yake kama Shia wanavyoitakidi, na kama hivi, na huu ni Mushkeli mkubwa inapasa wenye akili wa Kishia wafikirie. Mushkeli Mwengine: Kulayn ametaja katika kitabu chake (Al-Kaafii) Juzuu ya Kwanza ukurasa wa 239 ametaja Hadithi. Wametuhadithia wafuasi wetu wengi toka kwa Ahmad bin Muhamad kutoka kwa ‘Abdullaah bin Hajaan toka kwa Ahmad bin ‘Umar Al-Halabiy toka kwa Abi Basair amesema: Nilingia kwa Abu Abdillaah (‘Alayhis Salaam) nikamwambia: Nimekufanya mkombozi mimi na kuuliza mas-ala. Je, kuna yeyote anayesikia maneno yangu? Abu Abdillaahi akainua pazia lake, baina yake na nyumba nyingine akaangalia kitambo kisha akasema: ‘Ewe, Abu Muhamad uliza utakacho’. Nikasema, Mimi ni kombozi lako, kisha nikanyamaza kitambo kidogo, kisha akasema, kwa hakika kwetu kuna msahafu wa Faatwimah unajuaje Msahafu wa Faatwimah? Nikamuuliza: “Ni kitu gani hiki kinachoitwa msahafu wa Fatima?” Akasema: “Msahafu, ndani yake mna mfano wa Qurani yenu hii mara tatu! Wallahi hamna ndani yake yaliyomo ndani ya Qurani yenu hii hata herufi moja”. Sikiliza vizuri, Imamu anaapa na kusema, ‘WaLlaah hakuna herufi moja iliyomo kwenye Qur-aan yenu’ Nikasema: ‘WaLlaahi hii ni elimu’ akasema, ‘Ehee, Hakika hiyo ni elimu…’ Kwa hivyo: Je Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anajua msahafu wa Faatwimah? Kama alikuwa haujui basi ni vipi Ahlul Bayti waliweza kujua ilhali yeye hajui? Naye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Na kama alikuwa anaujua ni vipi aliuficha dhidi ya Ummah wake na Allaah Anasema: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake.” (5:67) Huu ni mushkeli mkubwa Enyi ndugu zangu tunataka jawabu. Mushkeli Mwengine: Katika Juzuu ya Kwanza ya kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn kuna majina ya watu waliopokea Hadithi toka kwa Mtume zinazotegemewa na Mashia Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na juu ya ali zake na Swahaba zake na amani, na wamepokea kauli za Ahlul Bayt miongoni mwao ni majina yafuatayo: hao ni wapokezi wa kitabu, ‘Al-Kaafi’ cha Kulayn watu waliopokea Hadithi za Shia, sikiliza vizuri majina na mnapata nini ndani yake? Mufadhal bin ‘Umar – Ahmad bin ‘Umar Halabi, ‘Umar bin Abaan ‘Umar bin Adhiinah – ‘Umar bin Abdil-Aziyz – Ibrahim bin ‘Umar –’Umar bin Handhalah – Musa bin ‘Umar – ‘Abbaas bin ‘Umar na jina lililokusanya majina yote haya ni jina la ‘Umar ni sawa sawa kama ni jina la mpokezi au jina la baba yake. Mushkeli ni kwa vipi hao wapokezi wataitwa kwa jina la ‘Umar nae ndie adui mkuibwa wa? Ahlul Bayt. Mushkeli Mwengine: Allaah Anasema: “…Na wabashirie wanaosubiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” (2:155-156) na Anasema tena, “…na wanao vumilia katika shida na dhara na wakati wa vita; hao ndio waliosadikisha, na hao ndio wajilindao.” (2:177) Subira ni jambo kubwa imetajwa katika Nahjul Balaaghah. Athari hii: ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akimhutubia yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Ali anasema kwa tamshi hili, ‘Lau usingekuwa umekata kubabaika na ukaamrisha subiri tungelia kwako maji ya Shani nyingi’ Hili limo katika (Nahjul Balaaghah) kadhalika katika (Al-Mustadrak) na imetajwa tena kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: ‘Mwenye kupiga mapaja yake wakati wa msiba basi amali zake zimepotea’, hili limo ndani ya kitabu “Al Khiswaal) cha Sudduuk ukurasa wa 621 na katika kitabu, ‘Wasaail Shay Twaan’.Ali ndio Imamu wa mwanzo kwa Shia ana waonya wafuasi wake akiwaambia: Mwenye kupiga mkono wake wakati wa msiba juu ya paja lake amani yake imeanguka, na vile vile Husain Imamu wa zama zake na Imamu wa dunia (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamwambia dada yake Zaynab katika Karbalaa kama alivyopokea mwenye kitabu ‘Muntahal Al-Aamaal’ kwa lugha ya Kifursi kimefasiriwa kwa lugha ya Kiarabu kinapatikana katika juzuu ya kwanza ukurasa wa 248. Husayn anasema: Na yeye ni Imamu wa tatu kwa Mashia akimuusia Dada yake Zaynab anasema: Ewe dada yangu, nakuapia kwa Allaah wajibu wako kuhifadhi kiapo hiki, nikiuwawa basi usichane nguo zako (kwa kulia),wala usiparure uso wako kwa kucha zako, wala usiomboleze maangamizi juu ya Shahada yangu (Kufa kwangu Shahid) anamuapia Allaah. Abu Jaafary Qamy amenakili: Kuwa amiri wa waumini (‘Alayhis Salaam) amesema katika ambayo wafuasi wake walikuwa anawausiana Hili liko katika kitabu “Man laYahdhuruhul-faqiih” na vile vile katika kitabu, ‘Wasaail’ cha Harul Al-Aamily, na tukihitaji kuainisha utajo wake Al-Hurul Aamiliy katika,‘Wasaail Shiiah’ Juzuu ya pili ukurasa wa, 916 Qamy ametaja ndani ya kitabu, ‘Man laYahdhuuruhul-Faqiih’ katika Juzuu ya kwanza ukurasa wa 232 Amiri wa waumini anawajuza wafuasi wake na anasema: ‘Msivae nguo nyeusi kwa kuwa hiyo ni vazi la firauni msivae nyeusi kwa kuwa ni vazi la Firauni’ na imekuja katika tafsiri Swaafy katika kutafsiri kauli yake Taalaa: “…wala hawatakuasi katika jambo jema…,” (60:12) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwabai wanawake kuwa wasivae nguo nyeusi, wala wasichane nguo wala wasinadi maangamivu, bali katika kitabu (Furu’ul-Kaafiy) cha Kulayn kuwa yeye alimuusia Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) akasema: “Mimi nitakapokufa usirarue uso, wala usiteremshe nywele wala usiniomboleze kwa maangamivu, wala usinisImamuishie maombelezaji” yaani usilete watu watakaoniomboleza kwa kupiga mayowe, na hili ni kama lilivyotajwa katika kitabu, ‘Al-Kaafii’ Juzuu ya pili ukurasa wa 528. Na huyu Sheikh wa Shia Muhamad bin Husain bin Babawayhi Al-Qamy aliyepewa jina la Suduuq kwa Mashia anasema: Katika matamshi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo hayakutanguliwa ni: “Kuomboleza (An-Niyaaha) ni katika amali za Jahiliya” kama wanavyopokea wanazuoni wao, Majlisy An Nuury na wanazuoni wao wengi toka kwa Mtume (Swalaah llwahu alayhi Wasallam) kuwa amesema: “Sauti mbili zimelaaniwa Allaah anazichukia mayowe wakati wa Msiba (Yaani mayowe wakati wa msiba) na kughani wakati wa neema” Swali na mushkeli ambao na wauliza wenye akili wa Mashia baada Ya riwaya zote hizi kwa nini Shia wanahalifu haki iliokuja na wanajipiga katika kumbukumbu yao katika Husainiyaat kwa kujitoa damu na kupiga na kuchana mifuko? Sasa tumkubali nani tuwakubali wao au tumkubali Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Ahlul Bayt wake watoharifu (Radhiya Allaahu ‘anhum). Utata Mwengine: Tatbiyr: Maana yake ni kujitoa damu kichwani kama wafanyavyo Shia katika Siku ya Ashura - nasema: Iwapo kujitoa damu na kujipiga vifua na kuchana nguo na kujiliza kwa sauti kuna ajira kubwa mbele ya Allaah, basi vipi Masheikh wenye kuvaa nguo nyeusi ambao ni kizazi cha Husayn (‘Alayhis Salaam) kama wanavyosema hawafanyi hivyo? Iwapo hili lina ujira kwa nini wao hawajitoi damu, kwa nini hawajipigi na kwa nini hawajimwagii damu nyusoni mwao? Hilo halifanywi isipokuwa na hao masikini ambao wanadhani kuwa wako katika haki, na wao sio hivyo kwa nini hawafanyi hivyo? Tunawataka wenye akili wa Shia tuwaulize swali hili na wajibu swali hili. Utata Mwengine: Ibada haiwi isipokuwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kujivunja na kujinyenyekeza katika daraja za kuabudu hakuwi isipokuwa kwa Allaah Taalaa; Allaah Anasema: “Bali Allaah muabuduni” Na hapa kuna mushkeli, kwa nini Shia wanajiita mja wa Husayn (AbduHusayn), mja wa ‘Aliy (AbduAli), mja wa Zahraa (Faatwimah) na mja wa lmam? Kwa nini hawakujiita hivyo Maimamu Ma’aswuum kama Hasan, Husayn, Sajaad, Kaadhim, na Maimamu Ma’aswuum kwa Shia? Kwa nini hawakuwaita watoto wao au kwa nini yeyote miongoni mwao hakumwita mwanae mja wa ‘Aliy, mja wa Zahraan, Je inaswihi kuwa maana ya Abdul Husayn yaani: Mtumishi kama wanavyohalalisha baadhi ya Shia? Wanasema: Abdul Husayn maana yake, mtumishi wa Husayn, Je anakuwa mtumishi baada ya kufa kwa shahidi Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) inaingiaje akilini kupelekewa chakula na maji na kumiminwa maji ya udhu katika kaburi lake mpaka awe mtumishi kama wanavyohalalisha hao masheikh (Al-Mu’amamiin) kwa waumini wao hao maskini, hili halifai. Utata Mwengine: Alipotawazwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) hatukumuona kutofautiana na Makhalifa waongofu kabla yake, na kuchukia uongozi, hatukumuona akimhalifu Abu Bakr, wala ‘Umar wala ‘Uthmaan hakuwatolea watu Qur-aan zaidi ya ile iliyokuwa kwao na hakupinga chao chochote, bali kauli zake zilikuwa nyingi juu ya mimbari. ‘Kheri ya ummah huu baada ya Nabii wake ni Abu Bakr na ‘Umar’ hakuhalalisha Mutah wala hakurudisha fadak, na hakuwahalalishia watu Mut-ah katika Hajj, wala hakuongeza haya njooni katika amali ya kheri –katika adhana wala hakuondoa – Swalaah ni bora kuliko usingizi– na kama Abu Bakr na ‘‘Umar wangekuwa makafiri walionyang’anya ukhalifa kwa Ali kama Shia wanavyodai, kwa nini hakulibainisha hilo aliposhika uongozi, na alikuwa na nguvu na ulinzi (Radhiya Allaahu ‘anhu)! Kwa nini hakubainisha na alikuwa na nguvu mkononi mwake? Bali kwa ukamilifu tumemuona akifanya kinyume cha hayo yote, aliwasifu wote wa tatu, na kawataja kwa wema aliposema: “Bora ya ummah baada ya Mtume wake ni Abu Bakr na ‘Umar” Nawaambia hao wenye akili, basi itoshe au itutoshe yale yaliowatosha nyinyi ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) pale alipowasifu wale watatu, (Radhiya Allaahu ‘anhum). Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Mu’aawiyah alikuwa kafiri, kisha tunamuona Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anajiuzulu ukhalifa na yeye ni Imamu Ma’aswuum, Imamu wa pili Hasan bin ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhuma) anajiuzulu kwa ajili ya kafiri mpinga dini, na hili ni kinyume na ‘Ismah kama mnavyodai au kuwa Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni Muislamu aliyestahili muadilifu. Mushkeli Mwengine: Ni kuhusu swali tunalolifikiria vizuri, na hiyo ni alama ya wazi kwa Shia kwa ujumla wake – Ithnaa ‘Ashariya (Maimamu kumi na mbili) swali linasema: Je, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisujudia kijiwe (turbah) cha Husayn ambao Mashia wanasujudia hivi sasa? na udongo huo unaitwa turba Karbalaa? Je Mtume alisujudia kijiwe kile? Ikiwa wanazuoni wa Shia watasema: Ndio, tutasema: Huu ni uongo hili halikuthibitika toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Leteni dalili zenu ikiwa nyinyi mnasema kweli na kama watasema. Hakusujudu, na hili ni kweli, tutasema: Ikiwa hili ni hivi, je nyinyi ni waongofu zaidi kuliko Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusujudia kijiwe cha Husayn, basi kwanini nyinyi mnasujudia udongo kwenye udongo wa Husayn kwa nyuso zenu? Pamoja na kujua kuwa mapokezi ya Kishia yanataja kuwa Jibril (‘Alayhis Salaam) alikuja na kifumba cha mchanga wa Karbalaa na imekuja katika baadhi ya athari, kuwa ardhi hii ni ambayo au imechanganyika na damu ya Husayn, au damu yake tohara (Radhiya Allaahu ‘anhu) imechanganyika na udongo huu, hapo alilia kama zinavyosema riwaya, kwa hiyo kwanini basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuusujudia? Je, Shia wameongoka zaidi kuliko Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Utata huu unahitaji jibu. Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa Swahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliritadi baada ya mauti yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakageuka baada Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Swali: Je Swahaba walikuwa kabla ya mauti yake walikuwa ni Ithnaashariah kisha wakabadilika kuwa Sunnah iliyosImamuishwa?”Au wao kabla ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa Ahlu Sunnah? Kisha wakabadilika kuwa Shia Ithnaashariah? Kwa kuwa kubadilika ni kutoka hali moja hadi nyingine tunataka jibu kwenye swali hili. Walikuwa Waislamu kisha wakaritadi wakageuka wakabadilika kama zisemavyo riwaya za Shia, kuanzia zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Je Swahaba walikuwa Shia Ithna ‘Ashariyah, kisha baada yake wakabadilika kuwa ahlu Sunnah au walikuwa ahlu Sunnah na juu ya Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakati huo ushia ulikuwa bado haujafahamika na kujitokeza? Tunataka jawabu katika hili. Utata Mwengine: Inajulikana kuwa Hasan (Radhiya Allaahu ‘anhu) yeye ni mtoto wa ‘Aliy na mama yake ni mwema Mtukufu Bi-Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) Na yeye ni miongoni mwa watu waliofunikwa (nguo) ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa Shia na yeye vile vile ni katika Maimamu Ma’aswuum Shani yake katika hilo ni shani ya ndugu yake Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu). Hapa kuna utata ambao tunataka utatuliwe: Kwa nini Uimamu umekatwa au kuzuiwa kwa watoto wa Hussan na ukaendelea kwa watoto wa Husayn? Baba yao ni mmoja mama yao mmoja na wote hao ni Mabwana, mabwana wa watoto wa vijana wa peponi, bali Hasan anamzidi Husayn katika jambo moja yeye amemzidi Husayn umri, na yeye ndiye mtoto wa kwanza kwa baba yake, kwa nini umekatwa na kuzuiwa kwa watoto wa Hasani nakuwekwa kwa watoto wa Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Utata huu unahitaji majibu na ufafanuzi na uchambuzi wa kielimu. Utata Mwengine: Kwa nini ‘Aliy hakuswalisha Swalaah japo moja katika maradhi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo amekufa ndani yake ikiwa yeye ni Imamu wa baada yake kama mnavyodai? Na kuwa jambo hili ni msingi katika misingi ya dini, halina budi lijulikane kwa mapokezi ya Mutawaatir bali hili ni asili katika asili za dini, kwa nini ‘Aliy bin Abi Twaalib hakuswalisha Swalaah hata moja katika maradhi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wala baada ya kutawafu kwake, kwanini hakuswalisha wala Swalaah moja? Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumwamrisha ‘Aliy bin Abi Twaalib kuswalisha hata Swalaah moja, na Uimamu mdogo ndio dalili katika Uimamu mkubwa na huu ni mushkeli. Utata Mwengine: Nyinyi mnasema: Sababu ya kupotea Imamu wenu wa kumi na mbili nae ni Muhamad bin Hasan Askary katika Saradib ni hofu ya dhulma, kama ilivyokuja katika riwaya zenu nyingi khofu ya dhulma basi kwa nini kupotea huku kunaendelea pamoja na kutoweka hofu hii, kwa kuwepo dola za Kishia kutawala kwa mujibu wa historia? Kama Dola Al-‘Abidiyiin Fatimiyah, Buwayhiiyiina, Swafin na mwisho ile dola ya Irani ya sasa ambayo nayo ina mitambo ya nyukilia, kwa nini asitoke hivi sasa? Na nyie mnasema ikiwa yeye hakujificha isipokuwa kwa hofu ya madhalimu na mashambulizi ya majabari, na zimekwishawahi kusImamua Dola za kishia jabari zenye nguvu, kwa nini asitoke sasa na kuna shia wenye nguvu wa kuweza kumnusuru, na kumlinda katika dola zao”? Bali kuwa mamilioni ambao wanajitoa roho zao kwa ajili yake asubuhi na jioni, tunataka majibu ya utata huu kwa nini hatoki? Utata Mwengine: Kulayn ameandika mlango maalumu katika, ‘Al-Kaafii’ kwa anuani! “Hakika wanawake hawarithi chochote katika ardhi” Imepokewa ndani yake toka kwa Abu Jaafar amesema: “Wanawake hawarithi chochote ardhini wala katika ‘Iqari kitu chochote.” Hili ni katika juzuu ya Suba ukurasa wa 127 katika kitabu, ‘Al-Kaafii’ cha Kulayn. Tunsi katika, ‘Tahdhib’ katika juzuu ya tisa ukurasa wa 254 toka kwa Maysarah kauli yake! Nilimuuliza Abu Abdillaah (a.s) kuhusu wanawake, nini haki yao katika urithi? Akasema, “Wao wanathamani ya tofali na jengo, mbao na Qaswab ama ardhi na ekari hawana chochote humo.” Toka kwa Muhamad bin Muslim toka kwa Abu Jaafar amesema, “Wanawake hawarithi ardhi wala katika ekari”. Na kutoka kwa Abdul Malik bin A’ayun toka kwa mmoja wao (‘Alayhis Salaam) yaani – mmoja wa Maimamu Ma’aswuum kwa Mashia – amesema:wanawake hawana chochote katika (“Ad-Dar wal ‘Iqaar” Nyumba na mali isiyohamishika kama vile ardhi na mashamba nk.)” katika riwaya hii hakuna uhusisho au kufunga, si kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) wala kwa Mwengine, juu yahili haistahiki kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) kudai urithi wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa riwaya ya Shia kwa kuwa Shia wanamkosoa Abu Bakr wanasema: kuwa yeye alinyang’anya urithi wa Fadak, au anachomiliki Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika mirathi yake katika Fadak pia kila lililokuwa la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hilo ni la Imamu zingatia kuwa imekuja katika riwaya za Kishia kutoka kwa Muhamad bin Yahya toka kwa Ahmad bin Muhammad toka kwa Amri bin Shammar toka kwa Jabir. Toka kwa Jaabir kuwa Abu Jaafar (‘Alayhis Salaam) amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah amemuumba Adamu akamkatia kipande cha dunia kwa hivyo lililokuwa la Adam (‘Alayhis Salaam) ni la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na lililokuwa la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni la Maimamu katika kizazi cha Muhammad.” Na hili pia liko katika ‘Usuulul Kaafi’ cha Kulayn ‘Kitabul Hujuh’ mlango kuwa ardhi yote ni ya Imamu (‘Alayhis Salaam) Juzuu ukurasa wa 476. Imamu wa kwanza baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa Shia ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa hiyo mwenye haki ya kudai ardhi ya Fadak ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na sio Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anha) na hatukumuoa ‘Aliy akifanya hilo, kwa hiyo tunataka jawabu kwa utata huu. Utata Mwengine: Ahlu Sunnah na Shia walikubaliana pamoja na tofauti yao kuwa Ali ni shujaa asiyeshindwa na kuwa yeye hakuhofia lawama yoyote kwa ajili ya Allaah. Na ushujaa huu haukukatika hata mara moja tangu mwanzo wa uhai wake mpaka alipouliwa kwa mkono wa Bin Muljam. Na Shia kama inavyojulikana wanatangaza kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib yeye ni wasii baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila upambanuzi wowote nae ni wasii wa moja kwa moja baada ya Mtume bila ya utata wowote. Nasema: Hapa kuna utata! Je ushujaa wa ‘Aliy ulikoma baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka ambai Abu Bakr kisha ambai baada yake ‘Umar kisha baada yake ‘Uthmaan bin Afaan, (Radhiya Allaahu ‘anhu) Je alishindwa japo mara moja katika minbari na akaogopa kupanda japo mara moja na kusema kuwa ukhalifa umeporwa kwake yeye, na kuwa yeye ndie mwenye haki, kwa nini hakufanya hivyo? Na yeye ndie wasii wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwanini hakudai haki yake?. Na yeye ndie yule shujaa ajulikanae na yeye alikuwa na wafuasi wengi wa kumnusuru wanaompenda, ambao watajazana pembeni yake la angelisema katika mimbari ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? kwa nini hakufanya hili (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Utata Mwengine? Hadithi ya Kisaai (shuka iliyowafunika watu wanne katika familia ya ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwasifu kwao kwa utoharifu. Wanne hao ni ‘Aliy, Faatwimah, Hasan na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhum) wote. Swali, ni ipi dalili ya kuwaingiza wengine katika utoharifu wa uhifadhi (‘Ismah) ikiwa Hadithi ya Mtume iko wazi kwa kuwa toharisha hao wanne, katika nyumba ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) Faatwimah, Hasan, na Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) wote? Basi ni ipi dalili ya kuwaingiza wengine katika utoharifu na Ismah na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuweka wazi isipokuwa katika hao wanne tu? Hili ni tatizo, tunataka jibu lake. Utata Mwengine: Shia wanapokea toka kwa Imamu Jaafari As-Swadiq (Radhiya Allaahu ‘anhu) nae ndio Muasisi wa madhehebu ya Jaafariyah kwa mujibu wa itikadi yao kauli yake akijifakhirisha anasema: Abu Bakr amenizaa mara mbili, mwangalie vizuri Jaafar As-Swadiq Imamu Ma’aswuum kwa Shia anasema! Abu Bakr amenizaa mara mbili, na hili lipo ndani ya kitabu cha, ‘Kashful-ghummah’ cha Al-Arbaly Juzuu 2 ukurasa wa 373, amesema: Abu Bakr amenizaa mara mbili, kwa vile nasaba yake kwa Abu Bakr imekoma kwa njia mbili ya kwanza: Kwa njia ya mama yake. Faatwimah binti Qasim bin AbuBakri ya Pili: Kwa njia ya bibi yake kwa mama yake Asmaa bint Abdi Rrahman bin Abu Bakr ambae yeye ni mama yake Faatwimah binti Qasim bin Muhammad bin AbuBakr, kisha tunapata Shia wanapokea kwa Jaafar As-Swaadiq riwaya za uongo za kumtukana baba yake Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) hili litakuaje? Swali Vipi Swaadiq atajifakhiri kwa babu yake upande mmoja? Na kisha kumtukana kwa upande Mwengine?!! Maneno haya yanaweza kutoka kwa mtu mjinga lakini hayawezi kutamkwa na Imamu ambaye Shia wanamzingatia kuwa msomi zaidi katika wakati wake. Kwa hiyo tunataka mkajibu juu ya mushkeli huu. Utata Mwengine: Shia wanadai kuwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wanazuoni wa Kishia wanadai katika Husayniyaat zao, kongamano na vikao vyao wanasema kuwa: ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy chuki kubwa mno, pamoja na hili tunapata kuwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) anatawalisha ‘Aliy Madiynah wakati alipotoka kupokaa funguo za Baytil Maqdis. Vipi yatakuwa haya? ‘Umar anamchukia ‘Aliy wala hampendi, na alipotoka ‘Umar kupokea funguo za Baytil Maqdis alimtawalisha Madiynah, naye ni ‘Aliy bin Abi Twaalib ambae hampendi na anamchukia sana, na kujua kuwa ‘Aliy atakuja kuwa Amiri wa Waislamu katika hali itakayomtokea ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa makuruhu yoyote yale. Yaani: Lau ‘Umar angeuwawa (Radhiya Allaahu ‘anhu) Ni nani ambaye angekuwa Khalifa wa Waislamu. Bila shaka angelikuwa ‘Aliy aliyepewa Uamiri wa Madina, Hili litakuwaje? Sasa vipi Shia wanadai kuwa ‘Umar bin Khatwab (Radhiya Allaahu ‘anhu) anamchukia ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha tunamuona ‘‘Umar anamtawalisha ‘Aliy uamiri wa Madina? Tunataka jawabu juu ya mushikeli huu. Utata Mwengine: Sikilizeni vizuri enyi Mashia wenye akili. Wanazuoni wa Shia wanaona kuwa viungo vya Swalaah ni vinane, paji la uso, pua, viganja viwili, magoti mawili, nyayo mbili, na viungo hivi vinapasa kugusa ardhi katika hali ya kusujudu na haya yametajwa katika kitabu cha, ‘Wasaail Shiah’ cha Hurul Al-Aamily Juzuu 3 ukurasa wa 598, kadhalika wanasema uwajibu wa kusujudu juu ya kisicholiwa wala kuvaliwa, kwa ajili hii wanaweka Turbah chini ya maji ya nyuso zao, chini ya kiungo kimoja katika viungo hivi nane. Swali: Kwa nini Shia hawaweki Turbah iliyochanganywa na damu tukufu ya Husayn chini ya viungo nyote vya kusujudu? Kwa nini wameukhusisha uso peke yake katika kusujudia udongo huu wa Karbalai? Na hali yakuwa nyinyi mmeamrishwa kusujudu juu ya viungo vyote vinane, paji la uso, pua viganja, nyao, na magoti. Kwa nini uso tu mlio wameukhusisha na huu udongo wa Husayn Karbalaai? Na hakuna dalili ya kuhusisha? Huku ni kupingana! Na utata huu tunataka jawabu. Imekuja katika baadhi ya riwaya za mushkeli Mwengine mfano wa kitabu (Al-Ghiibah) katika kitabu, ‘Al-Ghibah’ cha At-Tuusi: Kuwa Shia –wanadai katika baadhi ya riwaya kuwa Mahdi wao wa kumi na mbili ni Muhammad bin Hasan Al-Askari atakapo tokea katika Sirdaab yake Akhir Zamaan (Mwisho wa zama) hakika huyo atahukumu kwa hukumu ya watu wa Dawuud. Utata: Iko wapi shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yenye kufuta sheria zote zilizotangulia? Kwa nini anahukumu kwa sheria ya watu wa Daudi? Na shari’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iko wapi? Utata Mwengine: Sikilizeni vizuri, Shia wanaitikadi kuwa Maimamu wanabebwa na mama zao katika mbavu zao na kuzaliwa kwa mapaja yao ya kulia, kama alivyotaja Mas-uudi katika kitabu chake, “Ithbaat Al-Wasiyah” ukurasa wa 196: ‘Maimamu wanabebwa kwenye mbavu za mama zao na kuzaliwa kwenye mapaja yao ya kuume’ hapa kuna mushkeli na swali! Muhamadi si ndio bora ya Mitume wa mtukufu wa Maimamu na ni Mtukufu zaidi kuliko yoyote aliyewahi kukanyaga kwa unyayo wake ardhi hii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Yeye ndiye bora wa hao wote, kwa jambo gani alibebwa kwa tumbo lake na kwanini ametoka kwenye Mfuko wake wa uzazi? Kwa nini yeye hakutokea kwenye paja la mama yake la kulia?’ Huu ni utata unabainisha ghuluwi (kuvuka mipaka) na kupingana kwa kauli zao katika madhehebu hayana itikadi hii, tunataka jawabu la wazi la kielimu lenye kukata. Utata Mwengine: Shia wamepokea kuwa Abu AbdiIlaah Jaafar Swaadiq amesema: Mwenye jambo hii ni mtu hamwiti kwa jina lake isipokuwa Kafiri na hili liko katika “Al-Anwaar An-Nuumaniyah’ na imepokewa kwa Abu Muhammad Hasan Al-Askary kuwa amesema kwa mama yake Mahdi: “Utabeba mimba ya mtoto wa kiume, na jina lake Muhamad yeye atasImamua baada yangu” Je, huu sio mvutano hili limetajwa katika, ‘Al-Anwaar An-Nuumaaniyah’ ukurasa wa 55 Juzuu ya Pili yaani baada ya kurasa mbili za hadithi ya kwanza, kwa kuwa Hadithi ya kwanza ipo Juzuu ya Pili ukurasa wa 53. Na hivi sasa katika riwaya ya kwanza Abu Abdillah Jaafar Swaadiq anasema: Mwenye jambo hili ni mtu hamwiti kwa jina lake isipokuwa Kafiri.Yaani: Hatataja jina lake isipokuwa kafiri. Na tunaona kuwa Abu Muhamad Hasanal-Askary amesema akimwambia Umu Mahdi: Utabeba mimba na jina lake Muhamad naye atasImamua baada yangu, je huu sio mgongano? Mara mnasema: Mwenye kumwita kwa jina lake kafiri, na mara nyingine mnasema kuwa Hasan Askary alimuita kwa jina hilo Muhamad, Huu ni utata tunataka majibu. Utata Mwengine: Na swali jingine, lau mtu anataka kuwa Shia, Lau mimi nataka kuwa Shia hivi sasa ni madhehebu gani ambayo nitayafuata, au ni madhehebu yepi ninanayopaswa kuyafuata kati ya madhehebu mengi ya Kishia? Baina ya Imamuia Ismailiyah, kwa tofauti zao nyingi; Ismailiya Arkani au Ismailiya Mukarima au baina ya Ismailiya Buhrah na Ismailiya Nasiiriyah, au baina ya ‘Alawiya na Zaidiyah, au baina ya Duruuz, na makundi mengi ya Kishia. Kwa hiyo ni kundi lipi la Shia ninaloweza kulifuata, na kuliamini kwani yote yanajinasibisha kwa watu wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na wote wanakubali Uimamu wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na wote ni adui wa Swahaba na wote wanaitakidi Uimamu wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kuwa yeye ni nguzo na kuwa yeye ni khalifa baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila mwanya wowote ule, na kuwa pamoja nao wana asili ya dini na wanasifu Maimamu kwa hiyo ni madhehebu gani nitakayoyafuata? Imamuiyah Ithnaashariah? Au Ismailiya kwa aina zake au Naswiiriya Alawiyah? Au Duruuz katika baki ya Fatimiyah? Haya yanahitaji ithbaati. Utata Mwengine: Wakati Shia wanapotaka kuthibitisha Uimamu wa Ithnaashariyah wao wanatoa dalili ya Hadithi ya Kisaai ambayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja watu wanne tu swali: Faatwimah ametajwa kwa Hadithi Sahihi kwa uwazi kwanini amewekwa mbali na Uimamu na wala hatajwi katika Maimamu wa kishia? Hao wametajwa amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Aliy na Faatwimah Hasan, Husayn kwanini mmemtoa Faatwimah katika Maimamu kumi na mbili? Huu ni mushkeli unataka jawabu. Utata Mwengine: Kwa nini Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakupiga makofi alipokufa mwanae Ibrahimu? Kwa nini hakujipiga kama wanavyojipiga Shia, Mashia wanajipiga katika msiba wa Husayn na katika Husayniyaat zao? Na kwa nini ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye ni Imamu Ma’aswuum wakati wa kufa Faatwimahh (Radhiya Allaahu ‘anha) Kwanini hakujipiga? Hakujiparuza, wala hakujitoa damu? Hakupiga Qaamaati kwa minyororo au kwa mikono yake, kwa nini hakufanya haya na hiyo ni dini na hakuna budi itekelezwe? Tunataka jawabu juu ya huu utata. Utata Mwengine: Shia wanaitakidi kuwa Swahaba wengi walikuwa makafiri na wanafiki walioritadi isipokuwa wachache, na hili wanalolisema wengi wa katika wanazuoni wa kishia (Al-Mu’amamiyn – wenye vilemba), katika itikadi zao, na Mashia wenye akili wanakiri haya yote, ikiwa Swahaba waliriadi isipokuwa wachache mno miongoni mwao kuna waliokuwa wanafiki na baada ya mauti ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa watu saba tu, kwa sababu katika vitabu vya Shia kikiwemo cha Kulayni kuwa Swahaba waliritadi isipokuwa saba kwa hiyo waumini ni saba au kwa uchache wa hali ni wachache mno, kwa hiyo basi kwa nini basi hao walioritadi wasiwavamie na kuwashambulie hao wachache wanyonge, na kuwauwa wote? Na kwa nini basi hali haikurudi kwenye ukafiri na ujahiliya kama walivyokuwa babu zao na baba zao? Kwa nini hawa Maswahaba hawakufanya hivi? Nyinyi mnasema hao waliritadi na kuwa wao ni wanafiki walingojea mauti ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha wakaritadi wakamkufuru Allaah, wakarudi basi kwanini hawakurudi kwenye dini za baba zao Majahilia wa mwanzo, na kwanini hawakuwaua wale wachache waliobaki na imesemwa walikuwa saba au zaidi kidogo, hili linataka jawabu enyi Shia wenye akili, Utata Mwengine: Shia wanasema: Kulia juu ya Husayn ni Sunnah. Je, kulia huku kumejengwa juu ya dalili au hawaa (matamanio ya nafsi)? Ikiwa ni kwa dalili basi iko wapi dalili hiyo? Hili jambo moja, iko wapi hiyo dalili inayojuzisha kumlilia Husayn tukijua Husayn alimuusia dada yake asimlilie kwa kupasua nguo wala asijipige wakati Husayn atakapokufa. Dalili hiyo iko wapi? Kisha mbona hajafanya hivyo yeyote miongoni mwa Maimamu wa Ahlul Bayt ambao mnadai kuwa mnawafuata na mnaenda juu ya uongofu wao, tunataka jawabu. Utata Mwengine: Shia wanaamini kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni bora kuliko mwanae Husayn, na iwapo hali iko hivyo ni kwa nini hamumlilii kwa kukumbuka mauaji yake kama ambavyo mnalia kwa Husayn, nae aliyeuawa kama alivyouwawa Husein kwa nini hamlii kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mkajitoa damu mkajipa na kutoa rambi rambi kwa ajili ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Na yeye ni mtukufu wa wote? Na yeye ameuwawa kwa kupewa sumu na Mayahudi. Kwa nini msiba wenu huu mnauita Husayniyaati kwa nini msiunasibishe kwa Imamu wenu wa kwanza ‘Aliy na ukaitwa, ‘Alawiyaati au Muhammad ukaitwa, ‘Muhamadiyaati’ kwa nini mnaunasibisha kwa Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu)? Kwa nini hamfanyi Husayniyati aina nyingi au sehemu za kupokea rambi rambi, kama mnavyouita kwa Husayniyaati iteni ‘Alawiyaati, iteni Muhamad yaani iteni kwa majina ya Maimamu. Kwa nini hamfanyi hivyo.
Posted on: Mon, 25 Nov 2013 17:36:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015