kila mwenye maisha mazuri na uwezo wa kifedha, alipenda - TopicsExpress



          

kila mwenye maisha mazuri na uwezo wa kifedha, alipenda kuifurahisha familia yake kwa kutoka pamoja matembezini siku za mapumziko au hata sikukuu. Kuna waliopenda kubarizi katika upepo mwanana wa bahari huku wakigalagala katika mchanga mweupe wa pwani ya bahari ya hindi. Kuna waliopenda kuvaa nguo za ndani tu huku sehemu kubwa ya maumbo yao yakiwa nje. Kuna warembo waliovutia macho ya wanaume wakware waliozubaa wakiwatazama na watoto waliopenda kucheza ndani ya maji bila ya kujali kama waliweza kuogelea ama lah! Tofauti ilikuwa kwa familia ya Mzee Ngowi Nkoo. Siku hii ya sikukuu maalumu kwa wakristo duniani kote wakisheherekea siku ya kuzaliwa kwa bwana wao Yesu kristo aliyezaliwa miaka elfu mbili iliyopita, wao wakaamua kuimalizia katika msitu wa Gombe walipokuwa Kigoma kijijini kwa bibi yao mama wa mke wa mzee Ngowi, Zajiru Jibulenu. Ngowi ni mwajiriwa katika kampuni ya kutembeza watalii ndani ya mbuga za wanyama, hivyo hali ya kupenda kutembelea mbuga mbalimbali ilikuwa ndani ya damu yake na mishipa yake kusafirisha chembe chembe hizo kila sehemu ya mwili wake na kujikita katika ufahamu wake uliowaambukiza watoto zake. Alikuwa ni watoto watatu, Michael,Furaha na Janeth. Watoto hao nao, walifurahi sana kupata safari hizo za mbugani. walikwishatembelea Serengeti, Selous na Mikumi. Gombe ukawa ni msitu uliowatia hamaza zaidi kila waliposikia sifa zake. Kuna sokwe waliokuwa wakilea watoto wao kama anavyoishi binadamu wa kawaida. Hiyo ikawatia chachu kuwaona sokwe hao. Safari yao ilianza saa nane mchana, mara baada ya kula pilau na soda walizoandaliwa na bibi yao Bi Mwasiti Jibulenu. ...MSITU WA WAFU ...
Posted on: Tue, 20 Aug 2013 07:18:36 +0000

Trending Topics



n-left:0px; min-height:30px;"> Im 52 years old and I have seen more murders than you can possibly
GRUESOME WAY TO GO A Montreal woman died today after her
The TPP has been shrouded in secrecy from the beginning because
ALL INDIA BANK OFFICERS’ CONFEDERATION 4, Parliament Street,
Although i was too close to get much perspective on this cloud

Recently Viewed Topics




© 2015