kuwa deni kwa mhusika Akiwa ziarani mkoani Mwanza hivi karibuni, - TopicsExpress



          

kuwa deni kwa mhusika Akiwa ziarani mkoani Mwanza hivi karibuni, Rais Jakaya Kikwete amesema wale wote wanaombeza kuhusu utendaji wake, wataona aibu atakapomaliza muhula wake mwaka 2015. Kikwete amewananga pia baadhi ya wanaCCM wenzake kwa kushindwa kuyaelezea mafanikio ya Serikali yao. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme katika mikoa ya Mwanza na Geita unaofadhiliwa na Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC), Rais Kikwete alisema: “Wakati wa kampeni nilibezwa sana, lakini sasa ninawaomba walionibeza kufika vijijini na kuangalia ukamilishaji wa ahadi zangu. “Nataka waje waone, kwa sasa ninakamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vyote ili kufikia lengo la Watanzania asilimi 30 kufikiwa na nishati hiyo. Hadi 2015 umeme utakuwa umesambaa nchi nzima. “La umeme, leo nazindua nataka kuwaeleza walionibeza waje waone sasa ahadi zangu...hayo yote niliyasema kwenye ahadi zangu 2010.” Mradi huo umegharimu Dola za Marekani 15.54 milioni sawa na Sh24.87 bilioni kwa Mwanza na Geita pekee, fedha ambazo ni asilimia 25 ya Dola za Marekani 62.6 milioni sawa na Sh103.24 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 225 ya upanuzi wa njia za kusambazia umeme katika mikoa kumi nchini. Rais Kikwete alisema Serikali inajipanga kusambaza umeme na kufikiwa vijiji vyote na kubainisha kuwa mpango huo unakwenda sambamba na uanzishaji wa vyanzo vipya vya umeme ili viweze kuzalisha megawati 3,000 ifikapo mwaka 2015 na kwamba ziada itauzwa nje ya nchi. Kikwete akawageukia baadhi ya viongozi wa chama chake na kusema kuwa ni dhaifu katika uongozi kwani wameshindwa kueleza mafanikio ya serikali yao ya CCM. Ahadi za Kikwete 2010-2015 Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, Kikwete alitoa zaidi ya ahadi 70 na hadi sasa nyingi hazijatekelezwa. Zifuatazo ni baadhi ya ahadi hizo.
Posted on: Thu, 19 Sep 2013 21:50:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015