mwanamke mmoja alienda super-market kununua kuku, bahati - TopicsExpress



          

mwanamke mmoja alienda super-market kununua kuku, bahati mbaya kwenye frij kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mzani, akaonekana ana kilo moja na robo. mwanamke akamuuliza muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji akamchukua yule kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana ana kilo mbili. mwanamke akasema ‘Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie nawachukua wote wawili’ *Ungekuwa Muuzaji Ungefanyeje??
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 05:19:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015