story: sitaisahau dar es salaam mtunzi: mkweli wa kitaa mhariri: - TopicsExpress



          

story: sitaisahau dar es salaam mtunzi: mkweli wa kitaa mhariri: cox dawa yao mawasiliano: 0716746414 ilipoishia Nikageuka na kumuangalia baba, "mama yangu weeee, "" Nilijikuta naanza kupiga kelele baada ya kugundua yule niliyemchoma panga alikuwa ni mama yangu na wala sio baba... sasa endelea sehemu ya sitini na saba [67] nililia sana nilipogundua kuwa yule sio baba bali ni mama, nilipatwa na hasira sana na nikatamani hata kujiua na mimi, haikuwahi kutokea nikamuuzi wala kumfanyia kitendo kibaya mama yangu na sikutegemea kama ningemfanyia mama yangu vile, machozi, kamasi vilinitoka mfululizo huku macho yangu yakiwa mekundu sana, wakati huo wote nilikuwa bhado nimemkumbatia mama yangu na nikatamani hata utokee msaada ili nimuwahishe mama hospitali, japokuwa sikuwa na jua pale ni wapi lakini niliamini hospitali haziwezi kukosekana, wazo lakuwa pale ni ujinini sikuwa nalo japokuwa niliona maajabu mengi ila nilichokuwa na waza kwa wakati ule ni kumuokoa mama yangu tu. wakati bhado nipo pale nimemkumbatia mama ulitokea upepo mkali ambao sijawahi kuuona wala kusimuliwa tangu nizaliwe, upepo ule uliambatana na sauti za ajabu na vicheko pamoja na mílio isiyoeleweka, hivi vya sasahivi vilizidi yani ninaweza kusema ilikuwa mara mbili ya vile vya mwanzo, Upepo ule ulifika mpaka pale nilipokuwa na kwa kasi ya ajabu vikaanza kunipeperusha, nilijitahidi kumshikilia mama yangu kwa nguvu zangu zote ili popote upepo ule utakapoenda kunitupa niwe na mama yangu lakini ilishindikana, Nilianza kupeperushwa angani na mama naye nikaona anapeperushwa upande wake, nililia sana na nilijitahidi sana lakini upepo ulinizi nguvu kabisa, Kiukweli mpaka leo sijajua mama yangu aliperurushiwa upande gani wa dunia hii, ule upepo kiukweli hadi leo hii nikiufikiria bhado sijaupatia jibu, maana nilikuwa kama naelea angani ila sioni chini wala juu, wala sioni kitu chochote, akilini mwangu nilijua kabisa hii vita ni kubwa na sikuwa najua nitawezaje kuishinda, niliwaza kweli nahitaji msaada lakini sasa nani anayeweza kunisaidia?, Niliwaza sana huku niko hewani na sijui nielekeako hadi kichwa kikaniuma na nikaanza kupoteza nguvu taratibu taratibu, macho yakaanza kufumba taratibu kama mtu anayeanza kusinzia na nikalegea kabisa kiasi kwamba sikujua tena kilichoendelea, *********************************** Sauti za mawimbi ya maji ya bahari ndio iliyokuja kunistua pale nilipokuwepo, nakumbuka nilikuwa nimelala hivyo nikakurupuka haraka haraka ili nijue pale niko wapi, nilishangaa baada ya kuona bahari kwa mbele yangu umbali kama wa mita 50 kutoka pale nilipokuwepo, Nilianza kukumbuka taratibu taratibu nimefikaje pale na nilifikaje pale na ndipo nilipokumbuka kuwa niliomba msaada kwa jini Rahma ili nisifumaniwe, nikakumbuka vizuri maajabu niliyoyaona kule nisipokujua na jinsi nilivyomuua mama yangu mzazi, Nilijihisi labda nilikuwa ndotoni lakini je nakule baharini nimefikaje, woga ulianza kunijia tena na nikajichunguza vizuri kama nipo salama na mawazo ya kwenda nyumbani kwetu Tanga hata kwa mguu, kumbuka nilikurupuka lakinini nilikuwa sijasimama, nilipoangalia kule baharini niliona watu wakiwa kwenye mitumbwi wakiendelea na shughuri zao, mule pembezoni mwa bahari kulikuwa na watu wengi wengi ila kwa pale nilipokuwepo hapakuwa na watu, jua la jioni [alasiri] ndo lilikuwa linapotea upande wa magharibi na kwa mahesabu yangu ya haraka haraka nikajua ni jioni kama ya saa kumi na moja Nikakurupuka na kusimama ili nitafute msaada kwani sikuwa najua nipo mahali gani pale, niliponyanyuka nilijiangalia tena na nikajua nipo salama salimini, nilipopiga hatua moja mbele nikashangaa kuona karatasi nyeupe ikiwa imewekewa jiwe ili isipepeluke na upepo kwa pembeni yangu, nikataka kuipotezea ile karatasi lakini akili yangu ikaniambia niiangalie, nikaifuata mpaka pale ilipo, nikatoa lile jiwe na kuichukua, ilikuwa ni karatasi kama hizi za A4 na ilikuwa imeandikwa kwa maandishi mekundu, na mtu aliyeandika ilionekana alikuwa na haraka maana mwandiko wake haukunyooka, maneno yaliyoandikwa mule ndo yalinichanganya kabisa hadi nikakaa chini na nguvu zikaanza kuniishia ile karatasi ilikuwa imeandikwa kwa karamu nyekundu maneno haya; "FANYA HARAKA UENDE KWENU UKAMZIKE MAMAYAKO, ANAZIKWA KESHO SAA NNE ASUBUHI"" itaendelea kesho Gonga LIKE kama umeipenda SWALI: RAMA yupo ufukweni, je ni mahali gani? atakayepata atakuwa wa kwanza kuisoma hadithi ya kesho, 2ma jibu kene 0716746414 waweza #share au #comment kama ukipenda sponsored by: #NOLAN_MKWICHE
Posted on: Sun, 06 Oct 2013 13:13:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015