Abdullah bin Umar bin al-Khattab R.A.A amesimulia:"Siku moja - TopicsExpress



          

Abdullah bin Umar bin al-Khattab R.A.A amesimulia:"Siku moja nilikuwa nimepanda juu ya nyumba ya Hafsa (dadangu),nikamuona Mtume S.A.W Akikidhi haja akiwa ameelekea Shamu na kuipa mgongo al-Kaaba."Riwaya nyingine imesema:"ameelekea upande wa Baitul-Maqdis(Palestina)."Bukhary 148 Na Muslim 266. Anas bin Malik R.A amesimulia:"Mtume S.A.W Alikuwa akiingia chooni,basi mimi na kijana kama mimi tukibeba kiriba cha majina fimbo;Mtume S.A.W Akitamba kwa maji."Bukhary152 Na Muslim 271.Mtume s.a.w alikuwa akitembea nayo (fimbo hiyo)kwa sababu alikuwa anapomaliza kutawadha akiswali,kwa hivyo akihitajia kuikitisha mbele yake ili ipate kuwa ni kizuizi,anaswali kuielekea fimbo ile.(Sharhu Muslimya Nawawy).
Posted on: Tue, 25 Jun 2013 19:34:22 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015