ELECTRONIC FUND TRANSFER, ni njia ya kusafirisha fedha kati ya - TopicsExpress



          

ELECTRONIC FUND TRANSFER, ni njia ya kusafirisha fedha kati ya matawi ya Benki ya Posta Tanzania kwa mtandao. Jinsi ya kutumia Electronic Fund Transfer, nenda kwenye tawi lolote la Benki ya Posta Tanzania na utapewa fomu ya EFT ili uijaze. Kama unatuma fedha, mpatie afisa Benki ya Posta kiasi cha fedha unachotaka kutuma na fedha zako zitatumwa wakati huo huo. Mjulishe unayemtumia kiasi cha fedha kilichotumwa, tawi la kupokelea na jibu la swali la siri atakaloulizwa wakati wa kupokea. Kama mpokeaji fedha anayo akaunti, Benki ya Posta Tanzania, fedha zilizotumwa zitaingizwa katika akaunti moja kwa moja. Karibu Benki ya Posta Tanzania kwa huduma bora zaidi!!!
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 13:02:26 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015