Friday, November 1, 2013 BROOKLYN BECKHAM NA NDOTO ZA KUMFUATA - TopicsExpress



          

Friday, November 1, 2013 BROOKLYN BECKHAM NA NDOTO ZA KUMFUATA BABA YAKE. Brooklyin Beckham anataka kufuata nyayo za baba yake David Beckham kwa kufanya mazoezi ya majaribio katika klabu ya Manchester United. Brooklyn akifanya mazoezi na nahodha wa klabu ya PSG Thiago Silva wakati baba yake akiichezea klabu hiyo. Brooklyn akiwa katika jezi ya Los Angeles Galaxy ya Marekani wakati baba yake Beckham akicheza huko. Brooklyn akiwa na baba yake mwaka 2000 wakati Manchester United iliponyakuwa taji la Ligi Kuu. Hapa akiwa amebebwa na baba yake. Posted by beki3 at 3:47 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO. MECHI YA SIMBA, KAGERA YAINGIZA MIL 32 Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera iliyochezwa jana (Oktoba 31 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 32,726,000. Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 81 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 walikuwa 5,541 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,992,101.69, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,183,890 wakati kila klabu ilipata sh. 7,242,252.45. Wamiliki wa uwanja walipata sh. 3,682,501.25, gharama za mchezo sh. 2,209,500.75, Bodi ya Ligi sh. 2,209,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,104,750.37, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 859,250.29. VPL YAENDELEA RAUNDI YA 12Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo ipo katika raundi yake ya 12 inaendelea kesho (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji minne tofauti. Mgambo Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro). Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar. Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons. Posted by beki3 at 3:34 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook NEUER AFURAHI KUJIUMISHWA KATIKA ORODHA YA WATAKAOGOMBEA BALLON DOR. GOLIKIPA nyota wa klabu ya Bayern Munich, Manuel Neuer amesema amefurahishwa kuwa golikipa pekee kuchaguliwa kugombea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or mwaka huu. Neuer ni mmoja kati ya wachezaji sita wa Bayern walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 23 baada ya timu hiyo kufanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo katika msimu wa 2012-2013. Akihojiwa Neuer amesema ni heshima kubwa kwake kuwa golikipa pekee aliyepata nafasi hiyo na wote wanategemea kwamba mchezaji mojawapo katika Bayern ndiye atakayeibuka kidedea katika tuzo hizo. Bayern ambayo msimu uliopita ilikuwa ikinolewa na Heynckes, imeendelea kuwa katika kiwango cha juu chini ya kocha mpya Pep Guardiola toka kuanza kwa msimu mpya na Neuer ameeleza kufurahishwa na jinsi wanavyocheza hivi sasa. Posted by beki3 at 2:13 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook RAIS WA NIGERIA AMTUMIA MWALIKO BINAFSI ABU TRIKA. MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa zamani wa Misri na klabu ya Al Ahly Mohamed Abu Trika amepokea mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Nigeria-NFF kucheza mchezo wa kirafiki kwa ajili ya wahanga wa saratani Desemba mosi mwaka huu. Al Ahly ilitangaza kuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alimpa mwaliko binafsi veterani huyo katika soka. Kwa upande mwingine Al Ahly wamebainisha kuwa hawatamzuia nyota huyo kusafiri kwenda Nigeria kama timu itakuwa haina ratiba yoyote katika kipindi hicho. Abu Trika kwasasa yupo na timu hiyo nchini Afrika Kusini wakati wakijiandaa na fainali ya mkondo wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates itakayochezwa Jumamosi. Posted by beki3 at 2:11 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook ROMA YAWEKA REKODI SERIE A. KLABU ya AS Roma imekuwa timu ya kwanza kushinda mechi zao 10 za kwanza za Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A baada ya kuifunga Chievo kwa bao 1-0 jana. Katika mchezo huo Roma walijipaia bao lao la ushindi katika dakika za majeruhi kwa mpira wa kichwa uliopigwa na Marco Boriello. Roma chini ya kocha mpya Rudi Garcia aliyeanza kuinoa timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, imefikisha alama 30 katika msimamo wa Serie A, ikiwa ni alama tano zaidi ya Juventus na Napoli zinazoshika nafasi ya pili na tatu. Roma inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Torino Jumapili. Posted by beki3 at 2:07 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook NADAL, DJOKOVIC WATISHA MICHUANO YA PARIS MASTERS. MCHEZAJI nyota tenisi anayeshika namba moja kwa ubora dunia, Rafael Nadal na Novak Djokovic anayeshika namba mbili, wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Paris Masters baada ya kushinda mechi zao za mzunguko wan ne. Nadal alimgaragaza Jerzy Janowicz kwa seti 2-0 zenye alama za 7-5 6-4 wakati Djokovic alimtandika John Isner kwa seti 2-1 zenye alama za 6-7 6-1 6-2. Kwa upande mwingine Roger Federer naye alijihakikishia nafasi hiyo kwa kumchapa Philipp Kohlschreiber kwa 6-3 6-4 ambapo sasa atakwaana na Juan Martin Del Porto katika hatua ya robo fainali. David Ferrer, Del Porto na Thomas Berdych wataungana na Federer, Djokovic na Nadal katika msimu wa mwisho wa michuano ya ATP Tour jijini London mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Paris Masters. Posted by beki3 at 2:06 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook SERIKALI YA BRAZIL YAJIZATITI KATIKA USAFIRI ILI KUKABILIANA NA MSONGAMANO KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA MWAKANI. SERIKALI ya Brazil imesema itaongeza ndege pamoja na kuzindua njia mpya ili kukabiliana na foleni kubwa kwenye usafiri wa anga itakayokuwepo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Waziri anayeshughulika na masuala ya usafiri wa anga, Wellington Moreira Franco amesema serikali imepanga kuongeza ndege katika njia zilizopo na kufungua njia zingine mpya ili kupunguza msongamo wakati wa michuano hiyo. Kauli ya serikali imekuja kufuatia kilio cha wananchi waliokuwa wakilalamikia nauli kubwa ya usafiri wa anga katika michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka mwaka 1950. Tayari serikali ya Brazil imesikia kilio hicho na kukutana na wawakilishi wa mashirika ya ndege nchini ili kujadili utaratibu wa nauli inayoeleweka wakati wa michuano hiyo. Posted by beki3 at 2:04 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Older Posts Home Subscribe to: Posts (Atom) Search This Blog BBC NEWS FIFA - World Ranking TANZANIA - VODACOM PREMIER LEAGUE ENGLISH PREMIER LEAGUE STATS widgets Total Pageviews 110645 Blog Archive November (7) October (127) September (143) August (144) July (161) June (161) May (181) April (161) March (170) February (162) January (153) December (137) November (162) October (143) September (127) August (147) July (151) June (170) May (136) April (123) March (90) February (119) January (108) December (65) November (141) October (53) September (48) August (71) Simple template. Template images by Ollustrator. Powered by Blogger.
Posted on: Sat, 02 Nov 2013 04:18:45 +0000

Trending Topics



,900 -
Fourie Wedding - 27th September 2014 - Photos taken by
Se aclaro el misterio de los italianos.... ESPECTACULAR Y
I went up the village hall for a brunch with my neighbours and
I’m really curios to know how all of the pro Obama retired union
FS: Audio technica at2020 condenser mic.. 6500php (used but not
En polititjenestemann fra Telemark er siktet for forsettelig drap
I once posted this & since I am feeling nostalgic lemmie post it

Recently Viewed Topics




© 2015