Jana nchini Kuwait imeanza mikutano ya maafisa wa ngazi za juu kwa - TopicsExpress



          

Jana nchini Kuwait imeanza mikutano ya maafisa wa ngazi za juu kwa ajili ya kutaarisha mkutano wa kilele kati ya mataifa ya Kiafrika na Kiarabu utakaofanyika Kuwait Jumanne ijayo chini ya usimamizi wa Mfalme wa Kuwait Swabaah Al-ahmad Swabaah. Mkutano wa kilele utahudhuriwa na marais wa nchi za Kiafrika na viongozi na wafalme wa nchi za Kiarabu pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Nabil Al-arabiy na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Nkusuzana Dlamini Zuma Mkutano huo utajadili maswala mbalimbali kama ripoti ya harakati za Halmashauri ya Umoja wa Afrika na Kamati kuu ya Umoja wa nchi za Kiarabu, aidha mapendekezo ya kuimarisha nyenzo za utekelezaji wa mpango wa kazi ya pamoja kati ya nchi za Kiafrika na Kiarabu kutoka mwaka 2011 hadi 2016. CHANZO: Radio Cairo
Posted on: Fri, 15 Nov 2013 09:47:24 +0000

Trending Topics