Jana nilipata fursa ya kuchangia Bungeni, huu ni mchango wangu kwa - TopicsExpress



          

Jana nilipata fursa ya kuchangia Bungeni, huu ni mchango wangu kwa ufupi: >>>Bajeti hii ni pro-inflationary - inalenga kuleta mfumuko wa bei kwa sababu tumepandisha bei za mafuta, fuel, ambayo yanaendesha mitambo na hivyo kukuza bidhaa zinazozalishwa viwandani. Inapandisha kodi za mishahara wakati mishahara nayo imepanda, pia imepandisha kodi kwenye simu na kuanza kuchaji huduma zinazotokana na simu. >>>Badala ya kufanya hivyo tungetakiwa kupunguza kodi kwenye biashara ndogo ndogo kama vioski ili kuwapa motisha zaidi ya kuzalisha na kuwafanya walipe kodi wenyewe kwa hiari badala ya ilivyo sasa wanakwepa kodi na kuwahonga ma-ofisa wachache walafi wa TRA. Pia bajeti hii inashusha kodi kwenye mchele unaoagizwa kutoka nje mpaka kufikia 25% badala ya ile ya 100% - uamuzi huu utasababisha bei ya mchele wa ndani iwe juu zaidi kuliko ya ule wa nje hivyo kuondoa incentive ya wakulima wa ndani kulima kibiashara na hivyo miradi yetu ya umwagiliaji itakuwa haina maana yoyote ile. Badala ya kuweka mikakati ya kukuza uchumi wetu kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ndani - hata hizi za chakula - bajeti inaleta mapendekezo ya kuua uzalishaji wa ndani ili kuweka suluhu kwenye matatizo ya muda mfupi ya kushusha bei za chakula toka nje. Bajeti hii ni myopic na haina long-term visionary thinking ya kuleta maendeleo ya Taifa letu katika muda mrefu kama vile ku-stabilize balance of payment account kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kukuza uzalishaji wa ndani na hatimaye kudhibiti mfumuko bei. >>> Sikuunga mkono bajeti hii kwa vile imeshindwa kutoa majawabu ya changamoto zinazolikabili taifa letu - za ajira kwa vijana, njaa na usalama wa chakula, uharibifu wa mazingira, upatikanaji wa nishati endelevu, suluhu ya tiba dhidi ya maradhi, upatikanaji wa huduma bora kwa watanzania na udhibiti wa mfumuko wa bei. >>> Nilipendekeza ili niiunge mkono bajeti hiyo, serikali ifanye marekebisho kwenye maeneo niliyogusia, na ijikite kwenye kutengeneza bajeti ambayo itaongeza kipato kwa wananchi, itakuza uchumi, itakuza tax base, na iondokane na fikra kwamba ili tufikie ku-finance bajeti yetu ni lazima tuwakamue wananchi, badala yake tukuze wigo wa kodi, tuongeze compliance ya walipa kodi na tuweke tax equity kwa kuwachaji kodi stahiki wawekezaji wakubwa. Mwisho nilitoa wito kwa viongozi wenzangu wa kisiasa tuchunge ndimi zetu ili tulinde amani ya nchi yetu.
Posted on: Thu, 20 Jun 2013 06:01:31 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015