MCHEZAJI GANI ATAKAE VAA JEZI NO.7 Jezi namba 7,imekua na heshima - TopicsExpress



          

MCHEZAJI GANI ATAKAE VAA JEZI NO.7 Jezi namba 7,imekua na heshima kubwa sana ndani ya old trafford,kitu ambacho kimemlemea Antonio valencia na kuamua kurudisha jezi hiyo alie pewa na Sir Alex Ferguson. Valencia aliamua kuomba arudishiwe namba yake ya zamani #25. Valencia kwa kushindwa kuendeleza ushuja ulioachwa na walio vaa jezi hiyo,kina Eric Cantona,David beckham na Cristiano Ronaldo. Wafuatayo ni badhi wachezaji wanao weza kukabidhiwa jezi #7 WILFRIED ZAHA japo ni mapema kumjaji,zaha ameweza kuonyesha mwanga wa mafanikio haswa kwa mechi chache alizo cheza kwenye pre-season. kama ataweza kupewa nafasi na kuaminiwa msimu huu,bila shaka Zaha anawezo mkubwa wa kupewa jezi na.7 CRISTIANO RONALDO Maamuzi magumu alioyachukua Valencia ni dhahiri,kuna mchezaji mkubwa atapewa gezi hiyo. hatima ya Cr7,kuendelea kubaki njia panda,kama united watakubali kunja akaunti benki na kuamua kumrudisha ronaldo nyumbani O.T,hakuna shaka Ronaldo atakabidhiwa jezi yake ya zamani. GARETH BALE Baada ya mazungumzo ya Real madrid na Spurs kuvunjika,vyombo vingi vya habari vimeanza kuripoti united wameingia kwenye mbio za kutaka kumsajili. Kama atasajiliwa,Bale anauwezo wa kufanya makubwa akiwa na jezi namba 7. ROBIN VAN PERSIE Tangu asajiliwe amekua mchezaji wa kwanza kuvaa jezi #20.na kufunga magoli mengi kuwahi kuchezea united. licha ya Rvp kuahidi kuto badilisha na ya jezi yake,kutoka na mashabiki wengi walio nunua jezi yake,bado anaweza akatamanishwa kubadilisha namba ya jezi. anaweza akachagua kuvaa namba 7 au 9 ambazo zipo wazi.
Posted on: Tue, 13 Aug 2013 19:40:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015