Maajabu ya Tahiti Mwandishi Wetu Rio de Jeneiro, Brazil Toleo la - TopicsExpress



          

Maajabu ya Tahiti Mwandishi Wetu Rio de Jeneiro, Brazil Toleo la 299 NCHI ndogo yenye idadi ya watu 227,000 tu, Tahiti, inashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya Mabingwa wa Mabara inayoendelea nchini hapa na imekuwa kivutio cha wengi. Pamoja na udogo wake, tayari imeweka rekodi mbili katika mechi ya kwanza iliyochezwa juzi dhidi ya Nigeria. Kwanza, imefunga bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo na pili ikaweka historia ya kutoa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwa timu yake na kujifunga kwenye mechi moja tangu mashindano hayo ya mabara yaanze. Mchezaji huyo, Jonathan Tehau, ana stori nyingine ya kuvutia pia. Familia yake imetoa wachezaji wanne katika kikosi cha timu yao ya taifa ya soka. Mdogo wake, Alvin Tehau, ni mshambuliaji ambaye katika mechi dhidi ya Nigeria alicheza pia. Katika orodha ya wachezaji wa akiba waliokaa benchi wa timu yake, kulikupo na wadogo zake wawili. Kwa mujibu wa viwango vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Tahiti inashika nafasi ya 138 lakini hilo halikumzuia Tehau kupachika bao la kwanza la taifa lake katika michuano hiyo katika dakika ya 54 ya mchezo. Huku timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 3-0, Tehau aliruka juu na kumzidi maarifa mlinzi wa Nigeria, Efe Ambrose, ambaye anakipiga katika klabu ya Celtic ya Scotland. Baada ya mechi, Tehau alizungumza na waandishi wa habari na kusema mechi ile itabaki kuwa ya kukumbukwa kwa wananchi wa Haiti kwa maisha yao yote yaliyobaki. “Sisi ni nchi ndogo tu. Kwa kawaida tumezoea kuona mashindano makubwa kama Kombe la Dunia kupitia luninga tu. Leo na sisi tunacheza na mabingwa. Taifa zima linatazama. Kabla ya mechi rais wetu alitupigia simu na kutuambia ameahirisha kikao cha baraza la mawaziri,” alisema. Tahiti imepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya kuwa mabingwa wa bara la Oceania, linaloshirikisha nchi kama New Zealand. - See more at: raiamwema.co.tz/maajabu-ya-tahiti#sthash.js7KMbbW.dpuf
Posted on: Fri, 28 Jun 2013 10:28:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015