Na Ibrahim Yassin, Kyela MKAZI wa Kitongoji cha Mpunguti - TopicsExpress



          

Na Ibrahim Yassin, Kyela MKAZI wa Kitongoji cha Mpunguti (B)Kijiji cha Mpunguti kata ya Katumba songwe Wilayani Kyela Mkoani Mbeya Agoust Mwankinge( 36) anatuhumiwa na Serikali ya Kijij kwa kosa la kumbaka mtoto wakeSikujua Augost (16)na kumsababishia maumivu makali kwa lengo la kutaka utajili kwa imani ya kishirikina. Akizungumza na Tanzania Daima jana Kijijini humo mtoto huyo aliyetendewa kitendo hicho cha kinyama alidai kuwa wiki iliyopita Baba yake aligombana na Mama yake na kuamua kumfukuza na ilipofika saa 8 usiku Baba yake alianza kumtaka kimapenzi na alipomkatalia alimlazimisha kinguvu na kumsababishia maumivu makali. Alidai kuwa alipopata upenyo alikimbilia kwa Mwenyekiti wa Kitongoji ili kuomba msaada ambapo Mwenyekiti aliitisha mkutano wa wananchi na kujadili tukio hilo na kuwa aliwateua askari mgambo wawili kwa ajili ya kumsaka baada ya kupata taarifa kuwa alikimbilia Nchi jirani ya Marawi amabako walienda kumsaka bila ya mafanikio huku Mtoto huyo aliendelea kusema kuwa hii ni mara ya tatu kwa Baba yake kumuingilia kimwili ambapo siku ya kwanza alimueleza amsindikize kwa Dada yake anayeishi nchi jirani ya Malawi na walipokuwa njiani alimlazimisha kufanya naye mapenzi kinguvu kwa madai kuwa aliambiwa na mganga wa jadi kuwa akitaka kuwa tajili afanye mapenzi na mtoto ambapo usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tatu. Mama mzazi wa mtoto huyo Atupokigwe Killa alikili mumewe kumfanyia kitendo hicho mtoto wake na kudai kuwa alipopata taarifa hiyo alimuuliza mumewe ambaye alikanusha kufanya vitendo hivyo na baadaye alianza kumshushia kichapo na kumfukuza na kuwa alipoondoka tu usiku huo alianza kumtendea kitendo hicho mtoto na baadaye kukimbilia nchi jirani ya Malawi. Mwenyekiti wa Kitongoji hicho aliyekaimu Richard Mwakanyikisya alipopewa taarifa hiyo alimpeleka mtoto huyo kwa Afisa mtendaji wa wa kijiji Lusajo Mwakapiso ambaye aliandika barua ya kutaka mtuhumiwa akamatwe na aliawaita askari mgambo wawili John Mwankinge na Rashid Mwaipopo ambao walienda nchini Malawi ili kumkamata lakini walizuiliwa na Chifu wa kijiji cha mwambande kilichopo Wilaya ya Kalonga Malawi Green Mwangwala. Baada ya kukataliwa askari hao walirejea kujijini hapo na kutoa taarifa kwa afisa mtenda ji ambaye alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa hiyo katika kituo kikuu cha polisi Wilaya ya Kyela na kupewa Rb no KYL/IR/1768/2013 ambapo hadi hivi sasa wanaendele na jitihada za kumtafuta mtuhumuwa huyo na watamfikisha mbele ya vyombo vya sheria pindi watakapo mkamata. Wananchi wa Kijiji hicho kwa upande wao wamesikitisha na kitendo hicho na kudai kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha na vyombo vya sheria ili kutokomeza vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vinauashiri na vitendo vya kishirikina vinavyofanywa na vijana wengi kwa lengo la kutaka kupata utajiri wa haraka kwa njia ambazo si sahihi. Mwaisho.
Posted on: Sat, 10 Aug 2013 10:41:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015