Wakati mwingine moyo wako unahitaji FARAJA ili kuwa na FURAHA, na - TopicsExpress



          

Wakati mwingine moyo wako unahitaji FARAJA ili kuwa na FURAHA, na furaha ya moyoni inakufanya uonekani mchangamfu na mwenye KUTABASAMU, nalo tabasamu lako ni zawadi kwa wengine kuwasababisha nao watabasamu.Lakini ukimwona mtu mzima anatabasamu wakati yuko na shida nzito, jiulize inakuwaje mtu mwenye wakati mgumu ni mwenye furaha zaidi kuliko wewe unayemtazama ambaye hata umehuzunika na kuonyesha huruma kwake. Basi fahamu, ukiona mwenye shida kafurahi sio kwamba ametatua tatizo lake ila ametabasamu kwa kuwa amejipa moyo kuwa inawezekana na anajipa UJASIRI na kuonyesha UIMARA wake kutokana na shida aliyonayo na yuko tayari kupigana kiume kutatua shida. Ameweka matumaini ya kupigana bila woga hadi kushinda. Hivyo usikubali kupoteza tabasamu lako.
Posted on: Thu, 08 Aug 2013 13:39:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015